Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Timu za Tanzania Prisons ya Mbeya na Mlale JKT ya Ruvuma zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) uliochezwa leo (Aprili 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa.

Kwa sare hiyo Tanzania Prisons imefikisha point inane wakati Mlale JKT inazo tano. Timu tatu za kwanza katika fainali hiyo ya 9 bora zitapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao.

Mlale JKT ndiyo walioanza kufunga dakika ya 61 kwa mpira wa adhabu uliopigwa nje ya eneo la hatari na mshambuliaji Edward Malimi katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Shabani Shata kutoka Kigoma.
Dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho beki Richard Mwakalinga aliisawazishia Tanzania Prisons inayofundishwa na Stephen Matata baada ya kufanya shambulizi kubwa langoni mwa Mlale JKT.

Hadi tuna kwenda mitamboni, mechi ya pili kati ya Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City ya Mbeya ilikuwa ikiendelea huku Rhino Rangers ikiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 18 na kiungo Salum Tabayi.

Ligi hiyo inaendelea leo (Aprili 15 mwaka huu) kwa Mgambo Shooting ya Tanga inayoongoza ikiwa na pointi 11 kuivaa Polisi Tabora yenye pointi nne. Mechi ya pili itakuwa kati ya Polisi Morogoro yenye pointi kumi na Polisi Dar es Salaam yenye pointi sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...