Nimesoma sana hoja iliyotolewa kuhusu suala la kupokwa points Yanga, mimi binafi nimeipenda lakini ninachokiona ni kwamba mpira wetu unaendelea kupoteza radha, umevamiwa na Majuha wa soka ndiyo maana tunayumba sana, siyo siri hakuna statrehe kama kuangalia mpira wa ulaya, south Africa, Ghana, Nigeria bila kusahau Kenya ambako ligi zao zinaonyeshwa kwenye supersport.
Nasikitika kuona ujinga mkubwa unaendelea kushamiri kwenye mpira wetu, mara Uwanja wa taifa mara Zanzibar na kuna watu wenye upeo mdogo wako tayari kupigania hali hii iendelee kwa maslahi yao binafsi, athari zake ni kwamba tutaendelea kucheza hapahapa, hatutakuwa competitive kwenye mashindano yanayo jumisha nchi zilizojengwa kwa misingi imara ya football.
Hatuwezi kwenda mbele kwa kutegemea Uongozi wa akina Tenga, Tunapoteza muda wetu. Tunahitaji mawazo mbadala, fikra geuzi. tusione aibu kuiga kwa wenzetu waliondelea kimpira.
Ni Tanzania pekee ndiko mchezaji anaweza kumpiga refa au kupigana na mchezaji mwenzake lakini maamuzi yakachakuliwa baada ya mwezi au wiki kadhaa, usiniulize kwanini.
Kocha wa Italia hakumpa nafasi Balotteli kwasababu ya kufungiwa kijinga, lakini kosa amelifanya akiwa Man City. Tanzania ukifanya hivyo kwa mchezaji wetu kipenzi wa Yanga/Simba tutaandamana mpaka ikulu mchezaji wetu ooh imekuwaje, "bila huyu hatushindi sisi" "hapana lazima aitwe na acheze national team" na watangazaji uchwara kwenye viredio vyao nao watapiga kelele sana na kibaya zaidi mchezaji atapigiwa hata simu "ebwana haiwezekani sisi tunalivalia njuga lazima uitwe national team bwana"
Atacheza kwasababu hana nidhamu atapewa kadi nyekundu, mashabiki na watangazaji uchwara hawa wataanza kumsakama refa wa mchezo. is that football?? kwani na nyie watanzania mnataka kwenda mbele? kwa timu ipi? na wachezaji gani? hawa mnaowaokota wakiwa na miaka 30?eti mnawakuza ili wacheza baadaye!!! kwanini asipigane uwanjani?
mchezaji huyu hawezi kujua tafsiri ya kumsuma refa ni violence contact!!! Watanzania tumekuwa mijinga hatujui ethics za mpira basi mazuzu tu!! tunachekelea kila jambo la kipumbavu. Ninani anasema Tanzania mpira bila Yanga/Simba haiwezekani? au tumweka njaa mbele?
Tenga, nakuomba utambue umuhimu wa kuwa na professional company itakayosimamia mpira wetu, hizi siasa za CCM na CHADEMA tuondokane nazo tumechoka!! kama hutaki get out tuchague watu wenge vision nyingine. tunawadau wa mpira kama akina Jenerali Ulimwengu hapo Tanzania, how do we use them?
Jina Langu
Aman Awesu"AA"
Mkazi Wa Mafia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...