Ujumbe wa Serikali ya Taifa ya Mpito ya Libya, ukiongozwa na Mheshimiwa Mahdi M Gaziri (watatu kushoto.), Mkuu wa Ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali hiyo,ukiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete baada ya ujumbe huo kuwa umekutana naye Ikulu, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita (Picha na Ikulu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Vizuri JK wenzetu hawa Libya wanayo mafuta na wamekuwa wakichimba miaka nenda miaka rudi wakati sisi tunayo ila yapo ktk 'makabrasha' tukae nao vizuri Kibiashara ili tunufaike zaidi ya ilivyo kuwa enzi za Hayati!

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa Walibya smart guys sana na kwao wameendelea sana licha ya uharibifu uliotokana na vita mwaka jana, tukae nao vizuri ili tupate faida.

    ReplyDelete
  3. Mbona mnatuonyesha picha tu bila kutueleza sababu za ziara yao hapa kwetu? KULIKONI?

    ReplyDelete
  4. Kiko wapi?Nakumbuka wakati jamaa wanaelekea kuchukua nchi,kuna juha mmoja alikua anahojiwa na BBC,akaulizwa vipi uhusiano wenu utakuaje na nchi za ki Africa ambazo nyingi zimegoma kuutambua utawala wenu?Lile juha likajibu hao wanampenda Gadafi kwa kua alikua anawchotea bure mafuta ya walibya....na wala hatuwahitaji kuwa marafiki zetu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...