Na Zavara Mponjika
Namna gani watu wangu? Natumia fursa hii kufanya utambulisho mdogo wa jina la kona hii: Jicho La Ra. Pole kwa jamaa zangu wenye athari zinowakwaza kutofautisha herufi “L” na “R”. Ladha ya lugha ni matamshi.
Jina la “Jicho-La-Ra” lilikuwa ni jaribio langu la kuenzi wahenga wetu wa kale. Wanaofuatilia wanaweza kukumbuka nilirekodi santuri miaka ya 2003 (kwa sababu kadhaa haikutoka), na ilikwenda kwa jina hilo.
Nakumbuka moja ya waandaaji, Sani, mwenye asili ya Kinaijeria,  alishtuka sana baada ya kuona mantiki ya jalada la santuri ile, alisisitiza kuwa ile nembo ni ya ‘kishetani’.  Tuliingia kwenye mjadala mrefu na nikajaribu kufunguka naye, huku nikizingatia kwa kiasi gani mafunzo ya kigeni yalivyotufanya tushindwe kuthamini ama kusahau urithi wetu. Jicho la Ra ambayo ilikuwa na nembo ile ya asili, ilitufanya tufahamiane vyema hasa kuhusu mitazamo yetu ya ulimwengu; hiyo nembo ilikuwa ni utambulisho wa mafunzo ya ndani sana.
Ra au Horus kama alivyoitwa na Wayunani, ni moja ya mizimu ya kale sana na unaweza kusema moja ya nembo ya kiroho ya awali kuliko yoyote kwenye sayari hii. Urithi wetu wa utamaduni na maarifa mengine bado umebakia kule bonde la mto Hapi (unajulikana sasa hivi kama Mto Naili). Kule ndio mahala Wahenga wetu waliweza kufinyanga maarifa yote tuliyonayo leo duniani – imani, hesabu, siasa, teknolojia na mengineyo.

Kupata Stori Kamili BOFYA HAPA
"Tuko Sayari moja, tunaishi dunia mbalimbali
Maisha chemsha bongo, jaza mwenyewe."
Ra

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wewe umeanza kuwapigia debe kidogokidogo mashetani wenzako wa freemasons...ushindwe kabisa..sijaona ulichokiandika hapa zaidi ya upuuzi tu lakin najua sana adhari yake...sikubaliani na wewe hata chembe kidogo.

    ReplyDelete
  2. Tafadhali tumia njia nyingine ya kuwashawishi wasio na macho....lol. Nani asiye ijua hiyo alama ya FREEMASONS...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...