Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki , Mh Joshua Nassari kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma
Mbunge wa Busega, Mh Dr. Titus Kamani (mwenye kaunda suti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wanafunzi kutoka chuo cha Bugando, Mwanza, ambao walitembelea Bunge mjini Dodoma
Mbunge wa Busega, Mh Dr.Titus Kamani akisalimiana na madaktari wanafunzi wa Chuo cha Bugando, Mwanza ambao Aprili 18, 2012 walitembelea Bunge Mjini Dodoma
Ankoooo, pole na mihangaiko ya kutafuta ugali pamoja na kupotelewa na rafiki yako mpendwa kanumba,ila na sisi majonzi yalitukumba.LEO NAKUOMBA INIWEKEE HII KWENYE BLOGI YETU TUKUFU ILI WENZANGU NAO WACHANGIE HOJA. KWANZA NAWAULIZENI JE ? MMESOMA MICHUZI YA LEO TAREHE 19 , 2012 ANGALIENI MBUNGE WA BUSEGA AKISALIMIANA NA MADAKTARI WANAFUNZI WA MWANZA,SWALI LANGU NI FUPI SANA ,KWA NINI SIKU HIZI WATANZANIA TUMEKUWA WADOGO WADOGO SANA, JE ? MBEGU ZILE KUBWA KUBWA KAMA ZA MABABU ZETU ZIMEKWENDA WAPI ?? JAMANI HILI SWALI SIYO UTANI,IKO HAJA YA WANASAYANSI KUINGIA KAZINI KUFANYA UTAFITI,TAIFA LISIJE LIKAWA LA WATU WA MRABA MMOJA BADALA YA KUWA JITU LA MIRABA MINNE-HODARI NA AFYA ISIYOTISHWA NA KADUDU KADOGO KAMA MBU. ZAMANI HUKO MWANZA WALIKUWA WANAZALIWA WATOTO WA NGUVU AU KWA KISWAHILI CHA MWANZA (JILI TOTO) SIYO KATOTO.SASA JAMANI HIZI MBEGU NDOGO NDOGO ZIMETOKA WAPI ?? AU LISHE IMEKUWA NDOGO SIKU HIZI ??? NI MIMI ZEBEDAYO WA ZEBEDAYO (MWANZA)
ReplyDeleteVijana njaa tupu hamushibi ndiyo maana hamukui kisawasawa.
ReplyDeleteHalafu hiyo mbegu kubwa uwe mrefu mnene huwezi kutosha kwenye Hiace au Noah, itabidi uwe unatembea kwa miguu kila siku.
Naomba kuuliza: nguo aliovaa Mh. Nassari ni Kaunda suit? naona kama ina Chinese collar. Naomba nielimishwe.
ReplyDeletenimependa sana picha ya waziri mkuu na mbunge nassari wa arumeru, huyu nasari atakuja kuwa waziri one day. Natabiri
ReplyDeleteKwani hao madaktari wote wamezaliwa Mwanza??Usitake kutuchanganya nawe....Halafu hao madaktari wanafahamu madhara ya miili mikubwa unayoisema..so hao unaowaona hapo wanaitawala miili yao.Unapenda Kitambi na mafuta hey??
ReplyDeleteDavid V
Ndugu Zebedayo, pole kwa kutojua, wazee wetu walikuwa hawavunji amri ya sita kama sasa, sasa hivi amri ya sita kila mahali hadi kufanya unapomtafuta mtoto anakuwadhaifu/weak maana mizizi ilikuwa imechoka
ReplyDelete