KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA,SSP KIHENYA KIHENYA AKIZUNGUNZA NA ASKARI KATIKA VIWANJA VYA PALEDI.
MKUU WA UPELELEZI MAKOSA YA JINAI MKOA WA KIGOMA,SSP JOSEPHU KONYO AKITOA MAELEKEZO KWA ASKARI WAPYA KUTELEZA WQAJIBU NA SHELIA.
ASKARI WAPYA WAKIPEWA MAELEKEZO YA ULINZI SHILIKISHI.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanasheherekea sikukuu ya pasaka katika hali ya amani na utulivu, Jeshi la polisi limepanga mikakati madhubuti ya kupambana na uhalifu na wahalifu katika ngazi zote kuanzia vitongoji, vijiji wilaya na mkoa kwa ujumla tumepata Askari wapya wa kutosha .

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya Katika kipindi chote cha sikukuu ulinzi utaimarishwa katika maeneo yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko ya watu kuanzia katika maeneo ya starehe, sehemu za ibada, aidha wamiliki wenye vyombo vya usafiri wanakumbushwa kuzingatia wajibu wao wa kufuata sheria zote za usalama barabarani.

Kaimu Kamanda amesema kuwa wazazi wanakumbushwa kuhakikisha kuwa watoto wadogo wanakuwa na watu wazima wa kuwaongoza barabarani. kwa wamiliki wa kumbi za starehe wanakumbushwa kuzingatia kuingiza watu katika kumbi za starehe kulingana na idadi ambayo kumbi hizo zinastahili ili kuepuka misongamano ya watu inayoweza kuleta maafa.

Amesema Watoto wadogo wasiruhusiwe kwenye mikusanyiko ya usiku kwa mfano bar, na kumbi za starehe. Wazazi na wananchi kwa ujumla ni muhimu kuzingatia kwani hili ni swala la maadili. sanjari na hayo jeshi la polisi linawataarifu wananchi kwa ujumla kuwa hali ya usalama katika manispaa ya mji wa Kigoma ni shwari kwa sasa.

Kamanda Kihenya amesema hii inatokana na kudhibitiwa kwa matukio ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia nguvu ambayo yalitokea kati ya tarehe 15,16,17 mwezi march 2012. matukio hayo yamedhibitiwa na tangu wakati huo hakuna tukio la aina hiyo lililotokea. Niwatoe hofu Wananchi kupigwa nondo ni uzushi , wahalifu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. NDUGU YANGU ULIYEANDIKA NAOMBA RUDI SHULE UJIFUNZE KUANDIKA KISWAHILI VIZURI. SHELIA NA SHILIKISHI NDIO KITU GANI.

    ReplyDelete
  2. Afande SSP. KIHENYA KIHENYA na Kamanda SSP. JOSEPH KONYO

    Ahsanteni kwa Salaamu zenu za Pasaka na tunaahidi kutoa uhsirikiano mzuri kwenu.

    Usalama kwanza na Pamoja tulilinde Taifa!

    ReplyDelete
  3. Sajenti Chacha: Arooo pare, Koplo Mwita !!!!

    Koplo Mwita:NDIO Afande !

    Sajenti Chacha:ri-aresiti rire rikorofi ,riandikie RB na urisachi mifukoni,rivue mukanda,rivue viatu na uriweke rokapu!

    Koplo Mwita:Ndio Mkuu mara moja !

    ReplyDelete
  4. Sio Mchezo hawa ni wana wa Ras Makunjas.

    Kigoma endeleeni na Pasaka atakaeleta ujinga atakaa ndani kuanzia leo IJUMAA, JUMAMOSI, JUMAPILI, JUMATATU hadi hukooo Jumanne ndio atatoka kwa Dhamana !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...