Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. John Cheyo (katikati) wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zainabu Vulu. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akizungumza na mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Agustino Mrema wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Idd Azzan. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) Mhe. Zitto Kabwe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akiwa katika mazungumzo na katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue, wakati Balozi Sefue alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Katibu wa Bunge Nd. Emmanuel Mpanda, pamoja na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Ndg. John Joel.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza makamu mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) Mhe. Deo Filikunjombe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.Picha na Owen Mwandumbya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Haya Mheshimiwa Sefue, anza basi vitu vyako...maana bila kuangalia kwa ukaribu matumizi ya fedha za serikali hatuendi mahali Tanzania...ni kama kupiga ngumi ukutani.

    ReplyDelete
  2. bunge hili linaisha lini? na litakaa tena lini? uncle nisaidie

    ReplyDelete
  3. WIZI SASA BASI:

    Njia rahisi ni kuwawajibisha wabadhirifu wa Fedha za Umma kwa matumizi mabovu pia kuwajibishana kwa matumizi mabovu na sio kuipa Chadema utawala wa nchi!

    Bora Mawaziri wa Serikali ya C.C.M wawajibike kujiuzulu na tujirekebishe huku C.C.M iliyopevuka kuendesha Serikali ya nchi badala ya CHADEMA kuingia madarakani !

    ReplyDelete
  4. Hatuangalii chama sisi tunaangalia waadilifu. Chama si muhimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...