Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.


Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.


Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.

Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. La muhimu ni kwamba ujumbe umefika na sasa ni wakati wa mkuu wa kaya kufanya kweli, nae pia Pinda aanze kujeruhi makamanda wake kabla hajafikiwa yeye.

    ReplyDelete
  2. Ngoja nifunge mdomo..Lakini..narudia..Lakini...

    David V

    ReplyDelete
  3. Angekuwa SIX wangeipata hao vidokozi wa pesa za Umma.

    Ebu tuseme ukweli jamani..haya mambo ya kuoneana aibu Tanzania haitaenda kokote...Kuviziavizia vipengele kusaidiana hakutasaidia hata siku moja.

    ReplyDelete
  4. tutafika tu hata kama imepigwa chini, though justice delayed is justice denied, Mungu wetu ni mwaminifu na atawaaibisha tu hata mpeleke hadi december. Mafisadi lazima wawajibishwe.Cha msingi wenye ushahidi wajaribu kuusambaza na kwa wengine ili usichakachuliwe NAJUA MAONI YANGU HAYATAPOSTIWA HEWANI MAKE NI MSUMARI ILA NITAPATA PENGINE PA KUSEMEA SIKU HIZI NJIA NI NYINGI

    ReplyDelete
  5. HAMNA KILICHOHARIBIKA. UKWELI NI KUWA SIKU 14 HAZIPO MAANA BUNGE LINAISHA JUMATATU. ILA HOJA HIYO INAWEZA KUWAKILISHWA KWA SPEAKER JUMATATU, NA IKAWA IMEWAHI SANA KWA AJILI YA KUJADILIWA KIKAO KIJACHO!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...