Ndugu,
Ujumbe huu unakujia kwa sababu naamini wewe ni blogger.Sisi kama bloggers,tunawajibika kuwa na maadili au misingi yetu.Kinyume cha hapo kazi zetu,msukumo wetu unaonekana kuwa wa kiholela kama sio kihuni.Isitoshe,ni uonevu kwa wengine.Hapa nazungumzia maadili ya bloggers.Upo mchakato unaoandaliwa ili kuwa na maadili ya pamoja zaidi.Tunausubiri kwa hamu.

Lakini wakati tukiusubiri mchakato huo utimie,nimeona nigawane nawe maarifa haya(kizuri kula na nduguyo). Ni maadili ya bloggers.Nimeyachapa katika wavu wangu.Nakuomba ufuate kiunganishi hiki:



http://www.bongocelebrity.com/2012/04/30/zingatia-bloggers-code-of-ethics/#axzz1tR0bFGyq

Mwambie na yeyote yule ambaye unadhani anaweza kufaidika na ujumbe huu.Ukiweza uchapishe katika jukwaa lako. Pamoja tutafika.

Asante na uwe na siku njema

Jeff

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Hii ni nzuri.Nadgani itasaidia watu wengi.Maana kumekuwa na malalamiko ya kudhalilishwa ktk baadhi ya blogs.Na wahusika hawajil.Wengine wanafungua blogs,hata hawana malengo.Wanaishia kugombana na kila mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...