Makamu wa Rais, Dr. Mohamed Gharib Billal (kulia) na Balozi wa Korea,Mh. Young Kim wakikata utepe kuzindua Chuo cha Ufundi Veta,Mkoani Manyara kikiwa ni Chuo pekee kilichopo mkoani Manyara. Mkoa huo ni moja ya mikoa mipya ambao hauna chuo kingine chochote cha elimu yoyote zaidi ya hiki chuo cha Veta kilichozinduliwa leo.Uzinduzi huo, uliofanyikia katika mji wa Babati, umefanywa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal aliyeandamana na Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Philip Mulugo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Eng. Zebadiah Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi akimuonyesha Makamu Rais, baadhi ya zana za kilimo zitakazotumiwa na Chuo kipya cha Veta Mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    safi sana...huyu baba binafsi napenda sana....he must be VERY CLEAN!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...