Nimeguswa na kuumizwa sana na msiba wa ghafla wa msanii wenzangu wa tasnia ya filamu, Steve Kanumba, ndugu yetu, kijana wetu, rafiki yetu na mtanzania mwenzetu alietuachia pengo lisilozibika. 

Itatuchukua muda mrefu sana kusahau msiba huu wa taifa zima kutoka na umahiri wake, juhudi zake na kazi nzuri alizozifanya kwa kipindi kifupi cha uhai wake.

Nachukua nafasi hii pia kuwapa pole wazazi wake, mimi kama mzazi niko nanyi katika kipindi hiki kigumu sana, nimekuwa nawakumbuka sana katika sala tangu jana nilipopata habari hizi. Poleni sana

STEVE TULIKUPENDA, TUNAKUPENDA NA TUTAENDELEA KUKUPENDA, MUNGU AKUPOEE KWA AMANI NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE KATIKA JINA LA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU, AMEN

MRS CHRISTINA INNOECENT MAROLEN

MAMA BISHANGA

OHIO/ USA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...