MAMA MZAZI WA MAREHEMU (ALIYESHIKA TAMA) AMESHAFIKA JIJINI  NA AMETOA BARAKA ZOTE ZA MAZISHI YAFANYIKE HAPAHAPA JIJINI. WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE  AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA  KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE

 RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI. PICHA NA HABARI NA 8020FASHIONS


 MSALABA MWEKUNDU WAPO NA KAZI YAO INAONEKANA KWANI WATU WANAZIMIA MARA KWA MARA NAO WANAONEKANA KUFANYA KAZI YAO KWA USTADI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nipo nje ya Tanzania katika masomo tangu msiba huu utokee siwezi hata kusoma sikuwahi kumuona Kanumba live lakini kupitia filamu zake nilimkubali sana. Nakaa nawaza nahisi labda si ukweli labda ataamka, au walimuwahisha kumuweka kwenye fridge labda alipatwa hali kama ya mwamba hivi nachanganyikiwa. Nawapa pole wafiwa wote ila naposikiliza redio natokwa machozi. Mungu akulaze pema Kanumba. Tulikupenda Mungu kakupenda zaidi.

    ReplyDelete
  2. poleni sana wafiwa!!! mwanga wa milele umwangazie mdogo wetu kanumba, mimi nilikuwa naomba wale wanakamati wanaoandaa mazishi ya kanumba basi watoe angalau mda kidogo kabla ya mazishi kwa ndugu wa karibu tu kumwaga ndugu yao vizuri na sie taifa tukifuata, manake viongozi watawekwa mbele kabla hata ya ndugu au hata waende ndugu mwimbili hospital kwanza ndio waje na mwili ni hayo tu

    ReplyDelete
  3. nilikuwa nasoma, baada ya dakika tano nilitaka kujua global wana mpya gani ukurasa wa kwanza nilioukuta ni kuwa Kanumba katutoka , nguvu zilinisha niliona kama ndoto kwa kweli sina furaha naona kweli walimuwahisha kwenye frige i miss him napenda sana movie zake hana mpinzani huo ndio ukweli.mungu amlaze pema.

    ReplyDelete
  4. Mbona hatupewi taarifa za BABA YAKE MZAZI wa Steve?????? natoa hoja.

    ReplyDelete
  5. Tunataka kujua kwa undani taarifa za kina juu ya kifo chake. Natoa Hoja!!

    ReplyDelete
  6. Anonymous said...

    Mbona hatupewi taarifa za BABA YAKE MZAZI wa Steve?????? natoa hoja.

    Mon Apr 09, 08:14:00 PM 2012
    ______________________________

    ZITAKUSAIDIA NINI?? MUHIMU TUMLAZE SALAMA SK ACHA USHAMBENGA SAA ZA MATATIZO.

    RIP BRO

    ReplyDelete
  7. Geronimo Deuces-ChampionApril 09, 2012

    mbona hatupati habari za lulu? namwonea huruma kweli manake sijui hata atatokaje hata kama ni kuua bila ya kukusudia ni kesi nzito mno manake mpaka raisi kaenda ama kweli kanumba alikuwa mtu mkubwa.

    yote 9... kumi nimefurahi kuwa hichi ni kilio chetu wote kila mtu anajishirikisha kwa njia moja au nyingine.

    RIP kanumba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...