Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku mbili zilizopita nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akikumbatiana na Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba wakati alipofika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhani msiba huo,jioni ya leo.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimfariji Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba,Nyumbani kwa Marehemu,Sinza Vatican jijini Dar jioni ya leo.Kushoto ni Dada wa Marehemu Steven Kanumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. uchungu wa mwana....

    pole sana mama kanumba....

    pole sana wazazi wa lulu....

    manake wazazi wote ni kama wamepoteza watoto wao

    ReplyDelete
  2. Huyu Kijana alikuwa juu sana! Na Anawapenzi wengi hasa watoto wadogo ambao walipenda Movie zake! Ningeiomba Dr. Nchimbi ahamishie mziba huu uwanja wa Taifa ili vijana wengi waweze kuhudhuria au Wapitishe Mwili wa Marehemu Barabara kuu zote za Dar. poleni sana WaTanzania wenzangu.
    Amen
    R.I.P The Great

    ReplyDelete
  3. Yaani huyu mama nampa pole zote na kumuasa amshukuru Mungu kwa kile kilichotokea, aseme asante tu maana hukawii kumkufuru Mungu wakati wa matatizo.

    ReplyDelete
  4. Poleni Wafiwa pamoja na MAMA MZAZI WA MAREHEMU,

    Pia kilichobaki Mama Steven Kanumba atazamwe kama Mzazi wetu kuanzia kundi la Umoja wa Wanasanaa nchini na watu wote kwa Ujumla na isiwe ndio amekwisha mzika mwanaye moja kwa moja !

    ReplyDelete
  5. Mama Steven Kanumba aonewe huruma sana kwa kuondokewa na mwanawe pekee aliyekuwa anategemea matunzo kutoka kwake !

    Jamani kwa namna hii ni uchungu ulioje Mzazi huyu atakuwa nao?

    Mungu ampe Subira na Ujasiri.

    ReplyDelete
  6. Cha kuzingatia kikubwa ni kuwa SK anaondoka kipindi ambacho amepata mwelekeo wa kimaisha na Mafanikio baada ya kukutana na changamoto za kila aina na kujituma kwa muda hapo nyuma !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...