Na Ripota wa Globu ya Jamii.

BENDI ya Mashujaa Music imeendelea kuibomoa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambapo safari hii imewanyakua wanamuziki wake wawili ambao ni rapa Saulo John ‘Ferguson’ na mpiga tumba nguli Sudi Mohammed ‘MCD’.

Meneja wa Mashujaa Musica King Dodoo akiongea na Ripota wa Globu ya Jamii,alisema  kuwa wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika ushindani wa muziki ambapo wasanii hao wamejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.

Alisema pamoja na kuongeza nguvu katika bendi hiyo, wamewachukua wanamuziki hao kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao, ambapo Ijumaa hii wanatarajiwa kutambulishwa rasmi katika onyesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Busness Park, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa wasanii hao kila mmoja alisema ameamua kujiunga na bendi hiyo 
kwa ajili ya kuendel;eza kipaji alichonacho sambamba na maslahi mazuri ambayo wamepewa na watakayopewa pindi watakapokuwa wakiitumikia bendi hiyo.

“Kikubwa ni maslahi ndiyo yamenipeleka Mashujaa Musica kwani siku hizi kila mtu anaangali maslahi yake kwanza, pia nataka kuendeleza umahiri wangu katika upigaji tumba ,”Alisema MCD ambaye ameitumikia Twanga Pepeta kwa miaka 12.

Naye Ferguson tayari ametunga vibao vitatu kwa ajili ya mashabiki huku pia akitarajia kutambulisha mtindo mpya uitwao ‘Kibega’

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wajinga ,acheni kurubuniwa na visenti vya muda,mtamkumbuka asha baraka,kawatoa tongo tongo leo mnajiona ndo mmefika,kaeni chonjo kukosa ajira,mnamwiga dooodo,mwenzenu mzaire huyo

    ReplyDelete
  2. Kwani huyu Fagason si ametokea kwa Ali Choki (Extra Bongo) ama alirudi tena Twanga?

    ReplyDelete
  3. Tatizo kubwa la wanamuziki wetu ni kudanganyika na tamaa ya vitu kama simu za viganjani,mtu anaweza kuacha kibarua chake kwa muda kwa kuhamia bendi ingine

    ReplyDelete
  4. Twanga ni kisimi cha burudani mtahangaika weee ila mwisho mtarudi hapohapo.tena mama asha baraka sasa hivi ulitakiwa uiite Twanga Pepeta LTD mana imewasaidia wengi basi tu shukrani ya punda ni mateke.wacha wakimbilie vibendi vya msimu vinazuka na kufa ila Twanga tangu imepaa inakata mawingu tu.

    ReplyDelete
  5. NDIYO UTAJUA KWELI BENDI NYINGI AU BAADHI YA WANAMUZIKI HAWAONI KAMA MAJINA YAO YATAKUWA NA THAMANI AU KUUZIKA BILA KUSEMA WAMETOKA TWANGA PEPETA. ANGALIA HUYO FERGUSON ALIONDOKA TWANGA TOKEA 2009 NA KUHAMIA EXTRA BONGO MPAKA HIYO JANA.. BADALA YA KUTANGAZA WAMEMTOA EXTRA BONGO WANATANGAZA WAMEMTOA TWANGA PEPETA. AMA KWELI

    ReplyDelete
  6. Tokea wimbi la wanamuziki kuanza kurubuniwa na bendi mabali mabali na kuihama Twanga Pepeta na kwenda kuimarisha hizo bendi nyingina cha ajabu bendi zote ghizo zimeshindwa kusimama mpaka hii leo. Bendi hizo ni pamoja na Extra Bongo iliyochukua wanamuziki sita wakiwemo dancers, MAPACHA WATATU ilianzishwa ikiwa na wanamuziki wanne wa Twanga na sasa Mashujaa Musical wanao pia wanne tokea Twanga Pepeta. Cha ajabu zote hazijaweza kusimama huku TWANGA PEPETA yenyewe ikiwa bado imara na kuwatimulia vumbi kwa mbali. SIRI YAKE HAPA NI NINI WADAU?. Nashindwa elewa mie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...