ILE meli maarufu kama 'Meli ya Magufuli' ambayo Serikali ya Tanzania iiliansa katika Eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya kibali imenza kuzama baharini na imeharibika vibaya.
Inaelezwa kuwa Meli hiyo ya Tawaliq 1 Machi 8, 2009 ilikamatwa ikiwa na tani 293 za samaki aina ya Jodari iliyowavua katika bahari ya Hindi ndani ya Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), bila kuwa na kibali. Meli ya Tawaliq 1 ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia tamati ya kesi hiyo jumla ya wavuvi 20 walitiwa hatiani.
Lakini licha ya Mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu ilikuwa haijulikani na tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika Bahari ya India (IOCT) lakini meli hiyo imeanza kuzama kama inavyoonekana pichani. Kuzama kwa meli hiyo ni kutokana na kutoboka baadhi ya maeneo hivyo kuingiza maji ndani.
Inaelezwa kuwa Meli hiyo ya Tawaliq 1 Machi 8, 2009 ilikamatwa ikiwa na tani 293 za samaki aina ya Jodari iliyowavua katika bahari ya Hindi ndani ya Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), bila kuwa na kibali. Meli ya Tawaliq 1 ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia tamati ya kesi hiyo jumla ya wavuvi 20 walitiwa hatiani.
Lakini licha ya Mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu ilikuwa haijulikani na tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika Bahari ya India (IOCT) lakini meli hiyo imeanza kuzama kama inavyoonekana pichani. Kuzama kwa meli hiyo ni kutokana na kutoboka baadhi ya maeneo hivyo kuingiza maji ndani.
KUSEMA KWELI TANZANIA TUNA TIA AIBU. HILI TAIFA LINAELEKEA KUSIKO. HII MELI NI YA MAMILIONI YA DOLA INAOZESHWA KIUZEMBE. KWA NINI ISNGEKABIDHIWA TAFIRI AU MBEGANI WAKAITUMIA KWENYE TAFITI NA UVUVI? EE MUNGU TUNUSURU, EMBU WAAAMSHE HAWA VIONGOZI WETU MAANA HATA WEWE HUFURAHISHWI NA HII HALI. MUNGU TUSAMEHE MAKOSA YETU.
ReplyDeleteWakati taasisi ya utafiti ya TAFIRI ikiwa haina hata chombo kimoja chenye hadhi ya meli hii , na wala serikali haina uwezo wa kununua kwa sasa, ninashangaa kwanini wasipewe meli hii inayoozea baharini?? KWELI SERIKALI HAMNAZO
ReplyDeletewenzetu wakitaifisha wanatumia, sie tukitaifisha tunaharibu kama wehu......kweli aliyewalaani watanzania awaonee huruma wanataabika na hii laana.
ReplyDeleteserikali yetu inapenda kesi za kijinga ambazo matokeo yake zitaweza kuzalisha wadudu wa rushwa kuongezeka
ReplyDeletenina maana kusema hayo kwa mfano hao waliokamatwa kwenye meli hiyo itafika siku ya siku wataachiwa mmoja mmoja kutokana na uwezo wa utoaji rushwa
jambo la pili ukizingatia kuwa kama samaki walishavuliwa ni vyema kuwapa hao watuhumiwa onyo kali na kuwapa masaa 24 kuiacha nchi na kukimbilia makwao
sasa ukiangalia hapo watuhumiwa wataachiwa kwa njia ya rushwa na hapohapo watakuwa wametuachia uchafuzi wa mazingira baharini
hilo limeli litaleta uchafuzi wa mazingira na serikali haitojuwa ni wapi pakulipeleka sasa ndugu wadau hamuoni kuwa serikali yetu inapenda kujiongezea mizigo isiyokuwa na misingi?
Tunapotoka hatupakumbuki, na tunapo elekea hatupajui.. Tanzania imekuwa shamba la bibi..
ReplyDeleteHivi ina maana Mawaziri wote hakuna mwenye akili hata mmoja wa Kumshauri Raisi? Mbona mtu kama Membe, Nchimbi, Hussein Mwinyi, Sita wanaonekana wana busara wameshindwa kuweka kwenye AOB kwenye baraza la mawaziri?
ReplyDeleteSasa faida iko wapi, ni bora hiyo meli wangeachiwa hao wavamizi, maana samaki wenyewe hatuwavui, wanakufa kutokana na umri mkubwa, si bora watu wengine amabao ni wa Mungu wakafaidi kuliko hao samaki kuacha waozee baharini?
Nilichojifunza ni kwamba, viongozi wetu sehemu yeyote ambayo haina pesa hawashughuluki nao, wote macho yao yapo TRA, NSSF, Migodi, Vitalu vya uwindaji, kutembea na bundiki kujilinda, safari (perdiem), kumalizana kisiasa, uraisi 2015, posho, marupurupu, n.k.
Watanzania tumekwisha, hatutakaa tuendelee hata siku moja mpaka Issa ataporudi mara ya pili.
Hiyo scraper mnataka wapewe watafiti ili wazame nayo? Iache tu izame yenyewe
ReplyDeletehiyo meli si ingeletwa kigoma ifanye kazi ziwa tanganyika? Kigoma tunaweza.. angalia jinsi MV Liemba inavyodunda ingawa ni meli ya tangu vita kuu ya 1 ya dunia.
ReplyDeleteNasikia wameiba vitu kem kem toka kwenye hiyo meli na wakaamua kuitoboa izame kupoteza ushaidi. Niliona watu wa kigamboni wakitoa ushuhuda Mlimani TV kama sikosei. Walikuwa wakisema askari wamekuwa wakitoka na vitu mbali mbali including mafuta toka kwenye hiyo meli
ReplyDeleteKudadadeki kweli nchi imeoza viongozi wamevimbiwa na rushwa mpaka hawajui cha kufanya bye bye ccm 2015 mageuzi daima.
ReplyDelete