Kwenye Mitandao kijamii ya Facebook, Twitter kwenye eGroups na eForums.kumekuwa na Taarifa za kujiuzuru kwa baadhi ya Mawaziri wa Wizara mbali mbali nchini lakini taarifa hizi zinatofautiana na kwa kuwa hazijathibitishwa kwa namna yoyote ile, zitabaki kuwa TETESI tu. Ikiwa ni kweli itafahamishwa hapo baadae kwani vipo vyanzo husika vinavyotakiwa kutoa taarifa hizo!  

Unaweza kufuatilia mwenyewe kwenye ukurasa huu "bofya hapa"  utaona vijisanduku vya Twitter yenye tweets za Watanzania  na katika mitandao mingine kibao (Sio Globu ya Jamii).

Mojawapo inasema: "Wanaotajwa kujiuzulu ni Mkulo-Fedha, Dkt. Chami - Viwanda na Biashara, Dkt. Mponda - Afya na Nundu - Uchukuzi. Inasemekana watatoa tamko usiku wa leo."

    Joseph Msendo @msendo4life

    Breaking News ya Radio One, inasemekana mawaziri 8 wamejiuzulu..
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Nathan Chiume @chiume

    Unconfirmed reports of forced resignations of 8 ministers in #Tanzania by MPs from ruling caucus after opposition no confidence vote threat
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Edward Mhina @Mgossi

    RADIO ONE Breaking News: Inasema kwamba... Mhe.Jenista Mhagama ansema Wabunge wa CCM Wamefanya MAAMUZI MAGUMU usiku huu. Lakini HAJAFAFANUA!
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 20 Apr 12

    @Thuwein I claim no credit at all. Tunatimiza wajibu wetu. Players wengi, it was a teamwork @Semkae @Irenei2011 @iMashibe @AnnieTANZANIA

    Mbaraka Islam @Islam_Dar

    @zittokabwe @Semkae @MariaSTsehai @iMashibe Mkulo,Chami,Ngeleja, Nundu, Maige, Mkuchika, Maghembe Mponda barua usiku huu @ChangeTanzania
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

Nyingine inasema: " Mawaziri hao ni; Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda."

Sababu ya kujiuzulu inatajwa kuwa ni kumnusuru Waziri Mkuu na taratibu nyingine zinazochukuliwa pale Waziri Mkuu anapojiuzulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nawe waongea kama nani....si usubiri ukweli sasa. Au umetumwa??? unafurahishwa na serikali na mambo yake? Usituudhi

    ReplyDelete
  2. Uliyeandika posti hii,je unapendezwa na hizi kuwa tetesi au unapingana na wanaosukumia kujiuzulu kwa mawaziri hawa au unajaribu kusimamia ukweli na haki ya wananchi kupata habari sahihi?

    Kwa taarifa yako,ukiona habari hizi zinasambazwa ni vyema ujue kuwa hayo yatakuwa ni mapenzi ya wananchi wengi?Hakuna tetesi ambazo ni za kipuuzi zinaweza kusambazwa na wenye hekima ,elimu bora na uelewa lakini tetesi hizi zinazungushwa na watu ambao ni wenye stahi na mapenzi mema kwa nchi yao.

    Inabidi ufike wakati watanzania tuache ushabiki wa kisiasa na kuweka utaifa wetu mbele.Kama hawa mawaziri wanapaswa kuwajibika na hilo ndilo pendekezo la wananchi wengi basi ni vyema wakajiuzulu.

    Mpenda nchi.

    ReplyDelete
  3. WANG'OKE WAZIRI KAMA MAIGE KALIDANGANYA BUNGE,KAMDANGANYA WAZIRI MKUU NA KUHUSU BIASHARA YA VIUMBE HAI KWA KUSEMA KUWA TWIGA WALIOSAFIRISHWA KIA WALITOROLOSHWA WAKATI UKWELI ANAJUA WALIKUWA NA VIBALI HALALI VILIVYOTOLEWA NA IDARA YAKE,AMEWAINGIZA WAFANYA BIASHARA WAZAWA KWENYE UMASIKINI WAKUIFUNGIA BIASHARA HIYO GHAFLA HUKU AKIJUA WATU WANA LESENI WANA VIBALI HALALI VILIVYOTOLEWA NA WIZARA YAKE.LAKINI WAWINDAJI WAKUBWA AMBAO ASILIMIA TISINI WAENDELEE HII INAONYESHA MAWAZIRI HAWA HAWAKO KWA AJIRI YA WAZAWA,IMEHUZUNISHA JINSI TANZANIA INAVYOKWENDA INAONEKANA KUWA NI KAMA GARI BOVU LINALOKWENDA AMBALO HALIJULIKANI LITAFIKA SALAMA.MKULO NDIYO ANGETAKIWA AFUKUZWE KABISA MAANA NAMSHANGAA HATA RAIS WA NCHI HAKUCHUKUA HATUA YOYOTE KILE KITENDO CHA KUVUNJA BODI YA CHC WAKATI AMEIONGEZEA MUDA GHAFLA KABLA KIPINDI ALICHOIONGEZEA ANAIVUNJA ILI KUFICHA UKWELI WA TUHUMA HII NI KWELI ANAHUSIKA NDIYO MAANA ALIKUWA ANAFANYA KILA AWEZALO KUIVUNJA CHC ILI MAAMUZI MENGI YA MASHIRIKA YA UMMA YAENDELEE KUTOLEWA NA HAZIRI KUPITIA MSAJIRI WA HAZINA WAKATI CHC INA BODI AMBAYO INATAKIWA KUTOA MAAMUZI YENYEWE YA MASHIRIKA YA UMMA LAKINI SI MSAJIRI WA HAZINA ,WAZIRI WA BIASHARA AJUA UKAGUZI WA MAGARI KWA TBS NI WIZI NA KUWAONGEZEA WATANZANIA GHARAMA ZA UNUNUZI WA MAGARI UKWELI HAKUNA UKAGUZI UNAOFANYWA WANG'OKE

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe mtoa mada mbona kanjanja tu. Uelewa wako mdogo. Hizo link ulizozisema, kumeandikwa kua kuna tetesi ya idadi hiyo ya mawaziri kujiuzuru.Na wewe unasema habari hizo zibakie tetesi mpaka zitakapothibitishwa. Je, unapingana, au unakubaliana na habari toka link nyinginezo? Kuwa makini!!!

    ReplyDelete
  5. Thanks kwa kuweka mambo sawa. Ndiyo maana blog yako itaendelea kuwa juu siku zote, kwani wengine hawaelewi umuhimu kwa authenticated reports. Media haitakiwi kutu mislead bali kutuletea habari kamili za ukweli, uhakika na kwa wakati. Michuzi keep it up.

    ReplyDelete
  6. Media inafanya kazi na binadamu..Media sio machine. na hicho kikao hadi hatua ya hawa watu kupeleka barua za kujiuzuru hizi habari zimepeperushwa na wenzao hao hao. Wenye mapenzi mema. Lisemwalo lipo kama halipo linakuja. Uozo mtupu.

    ReplyDelete
  7. keep it up ankal. watu sijui wana kiherere gani si msubiri vyombo husika vitoe rasmi habari hii. Sasa mnamtaka Michuzi aconfirm as who? msiwe tu wafuasi kama wa kony vile hata hamjui mnachokifata

    ReplyDelete
  8. Tunazidi kuwa Taifa la wambea na waongo tu. Inasikitisha zaidi watu wenye nyadhifa Kama Mhe. Zitto nao wakiwa chombo cha kueneza umbea huo!

    ReplyDelete
  9. mnataka kushikana mashati humu,tulieni jamani ukweli atatupostia ankal,ila kwidodomya kunawaka moto.KWELI

    ReplyDelete
  10. Imbombo ngafu

    ReplyDelete
  11. "Wahenga walisemaga lisemwalo lipo na kama halipo linakuja" Tusubiri wakati ufike, watanzania hatuna imani tena na hao mawaziri na wala hatuwahitaji katika serikali yetu wamefanya madudu ya kutosha wapumzike na wakafanye shughuli zao binafsi tunawapa ruhusa. Ila wakibainika kwamba wamefuja mali ya umma lazima wachukuliwe hatua za kisheria na wawajibishwe kwanza kwa kufilisiwa mali zao na zirudishwe kwa wananchi, kwani hizo pesa zote zipo kwenye accounts zao za ndani na nje ya nchi uchunguzi ufanyike yatabainika makubwa zaidi!

    ReplyDelete
  12. Hii blog ya Ankal siyo ya kisanii na haifanyi kazi kwa kudhania na kwa tetesi, huyo aliesema kuwa hakuna tetesi za kipuuzi zinazoweza kusambazwa na wetu wenye hekima, elimu na uelewa, mbona hadi sasa ni tetesi ukweli hakuna. Mtu yoyote mwenye elimu iwe elimu dunia au elimu akhera hawezi kukurupuka tu na kusema tu neno asilokuwa na uhakika nalo, tumeambiwa na Mwenzi Mungu……….’ Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. [17:36] mtakuja sutwa, mnatokwa na fahamu bure, kwani wakishaondoka hao 8 kisha inakuwaje ndio mbingu na ardhi vitafunga? Huo sasa ndio ushabiki wa kisiasa, kama watajiuzulu watajiuzulu tu, ushabiki wa kutandaza habari zisizo za kweli inahusu nini, mmeumbuka na hiyo mitandao yenu. Na unatumia kigezo gani unaposema haya ndio matakwa ya wananchi, matakwa ya Zitto, Chadema na wenzie sio matakwa ya wananchi, tatizo mna papara sana mbona 2015 bado? Tuombe uhai na uzima tu kwa Allah (SWT) simbali ukweli utadhihirika na uongo utajitenga.

    ReplyDelete
  13. hongera wabunge vijana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...