Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘lulu’ akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
 Msanii huyo anatuhumiwa kuhusiana na  kifo cha msanii nguli wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba.
Msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' akiongozwa na Askari Magereza kuingia ndani ya gari baada ya kutajwa kwa kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo.


                                                   Lulu (katikati) akilindwa na askari lukuki
                                              Lulu akiingizwa rokapu ya Mahakama ya Kisutu
                       Lulu akiwa ndani ya basi la Magereza tayari kupelekwa gereza la Segerea
 Askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakilinda msafara wa mahabusi akiwemo Lulu
Askari Magereza wakifanya doria nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.

Kamishna wa tume ya haki za binadam, Joaquine De - Mello leo amejitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiambatana na mawakili wengine wa kujitegemea kumtetea msanii ya sinema, Elizabeth Michael aka Lulu.


Akilitaja jopo la mawakili wanaomtetea Lulu, wakili wa kujitegemea Kennedy Fungamtama, alisema kuwa mama De Mello ni miongoni mwa mawakili pamoja na Furgence Masawe na Peter Kibatala. Hata hivyo hawakuongea lolote mahakamani.


Wakili wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kuwa kesi imekuja kutajwa.Hata hivyo, alisema,  upelelezi bado haujakamilika na kwamba anaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Ikapangwa kutajwa tema Mei 7, 2012.


Awali hali ilikuwa mshike mshike kumpitisha Lulu kutoka chumba cha mahabusu kumleta chumba cha mahakama kwa sababu watu walikuwa wengi pamoja na wanahabari waliokuwa wakimuwinda kupata picha yake.


Korido ilikuwa ndogo kutokana na msongamano wa watu.  Lulu alipitishwa akiwa amezungukwa na maaskari magereza bila shaka  kuzuia asiguswe na watu au kumfanya jambo lolote.


Baada ya purukushani hiyo ya nguo kuchanika, aliingizwa mahakamani akilia kwa sauti kutokana na usumbufu alioupata kutokana na mbanano uliokuwepo,  jambo lililolazimisha mlango wachumba cha mahakama kufungwa na watu kusukumwa nje.


Ikamlazimu Hakimu kutoa amri kuwa kesi hiyo iwe inasomwa mapema zaidi na kuwaamuru  maaskari kuwaondoa watu wote ndipo atolewe kurudishwa mahabusu bila usumbufu tena. Alimpa  Pole Lulu kwa usumbufu alioupata.


Baada ya kutoka Kortini Lulu aliyekuwa amejitanda ushungi, alipelekwa kwenye gari na kuondolewa kwa kasi eneo la mahakama hiyo kwa basi  la magereza, akiwa mfungwa pekee kwenye gari ile iliyojaa pia askari magereza waliokuwa wakimlinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Asante Blog ya Jamii na hasa aliyekuwa amepangwa kuleta coverage hii pamoja na picha..Picha zinaonekana zilikuwa kazi kweli kweli kuzipata, zilihitaji utaalamu wa ziada kuzipata na Kamera "ya Ukweli".Keep it up blog ya jamii..Tunasubiria na Dodoma.

    David V

    ReplyDelete
  2. Amezungukwa na maaskari magereza WENGI mno, sio lazima, security is too tight for a delicate 18 (17?) year old like that...

    ReplyDelete
  3. Lulu akimaliza kesi mi niko tayari kumpa hifadhi ya maisha huku kwangu.(Norway)

    ReplyDelete
  4. Ulinzi kwa kweli ni muhimu. Huyu binti yupo hatarini sana. Wapambe wa marehemu bado wako na hasira. Wakifanya mchezo tu wakamwachia mapema, ni rahisi kugawanywa vipande-vipande.

    ReplyDelete
  5. Lulu anahitaji ulinzi wa kutosha kwa kweli.

    ReplyDelete
  6. Huyu binti wanamuonea tu. Knaumba kafa bahati mbaya kadondoka kajigonga kichwa!

    ReplyDelete
  7. Anatia huruma sidhani kama kuna kesi hapo ya kujibu aachiwe huru tu

    ReplyDelete
  8. sikujua kama vazi la hijabu ni muhimu kwa mungu pale unapokuwa na shida pole sana binti kesi haina ushahidi wa kutosha usihofu naomba aletwe kwangu huku UNITED KINGDOM kupata hifadhi

    ReplyDelete
  9. james lerombo,,,,,(jimmy wa ukweli),,,me roho inananiuma sana,,,,kama vile wanamuonea tu huyu binti,,,,sheria naona inakosea sasa,,wiki mbili tena za mateso kwa lulu,,,,hii sio nzuri aseee,,,,so pain to guyz,,,,

    ReplyDelete
  10. kahh kumbe, si alisema akivaa nguo ndefu anawashwa leo vip. mama akisema vaa nguo ndefu mwanangu alijibu kwa jeuri namna hiyo.

    ReplyDelete
  11. Jamani huyu binti anatia huruma, ila katika muonekano fulani anaonekana kama mjamzito, labda ni picha lakini mmh tusubiri siku ziende tuone.

    ReplyDelete
  12. jamani mnaosikitika mbona mnapendelea,mtoto wa babu seya alikuwa chini ya miaka 18 na alikaa segerea muda mrefu mbona hamkusema wala wakili yeyote hakutokea kumtetea???.acheni sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  13. sawa anatia huruma lakini lazima tukumbuke kuwa familia ya SK pia inataka kupatwa na "closure" tusiseme tu anatia huruma tujiweke na sie kwenye upande wa mama Kanumba je ingekuwa wewe ungemwachia tu?

    Hivi ni vilio viwili kwakweli kwa mana hata akitoka vidole vitakuwa kila leo na ustaa ndio umeisha tena

    ReplyDelete
  14. msiangalie uchungu wa upande mmoja. hata ndugu zake kanumba nao wanaumia. acheni sheria ichukue mkondo wake ili kubaini kama ana kosa au la. sio mnakimbilia kusema tu kaonewa. je mnajua ukweli? anayejua ukweli ni lulu peke yake hivyo maelezo yake ndio yanafanyiwa kazi na mimi na wewe hatuyanui maelezo hayo kwani sio kilakitu kinawekwa hadharani.

    ReplyDelete
  15. SCAPE-GOAT!!!

    ReplyDelete
  16. Uliesema uja uzito na mimi naafiki pia, huyu mtoto ni mjamzito. ngoja tuone

    ReplyDelete
  17. UPANDE WA PILI WA SARAFU:

    ''TUHUMA ZA LULU KUHUSIKA NA MAUAJI''

    Kinachomgharimu huyu Binti ni kuwepo eneo na muda Kanumba akifariki, huku mazingira ya kukwaruzana yakiwepo.

    Marekani ilitokea mwana 1989 Kijana mmoja (Mtu mweusi) alikuwa anatoka nje na Mgahawa alipofika mlangoni akaanza kukwaruzana na Mlinzi (Mzungu) ghafla ilitokea risasi kutoka kusikojulikana ikatua mwilini mwa Mlinzi (Mzungu) akafa papo hapo, Kamera za usalama zikachukua ikaonekana yule Kijana Mweusi ndio muuaji kumbe siyo kabisa na Kesi hii iliendeshwa ikitolewa hukumu mara kadhaa na R ufaa kukatwa kupinga hukumu hadi mwishoni mwa mwaka jana baada ya miaka 22 Hukumu ikatoka Mahakama Kuu ya Marekanei Kijana akanyongwa!

    Mazingira hayo ndio kama suala linalomkabili Lulu kwa sasa, hivyo pana umuhimu wa kuangalia Upande wa pili wa Sarafu!

    ReplyDelete
  18. Hao haki za binadamu katika kesi hii ndo wanaona umuhimu wa kutafuta na mawakili? mbona kuna human rights abuses kibao hawatokei kusaidia watu? wamama wangapi wanaumizwa hatujawahi kuwaona mawakili wanajitokeza? albino wangapi wameuliwa hatujaona wakili akijitokeza ama ndo chance ya kutaka kukuza jina kwa vile case imevuta wengi? tendeni hizo haki kwa watu wote na pia mfikirie haki ya SK ya kuishi

    ReplyDelete
  19. Ivi nyie mbona kama kweli nyie mnahuruma mbona sioni mtu anaeemzungumzia Mama Kanumba kwa uchungu wa kumpoteza mwanae milele?

    Na mbona mtoto wa babu Seya kijana mdogo chini ya miaka 18 mbona hakutokea mtu wa kupiga kelele na kumtetea kijana yule

    Halafu nyie watu wa haki za binadamu hamna haki yoyote nyie ni wanafiki wakubwa kuna watoto wangapi wapo magerezeana na hamjawatetea? mtoto wa babu Seya nani alimtetea acheni unafiki na mumwogope Mungu na muache huo ukabila wetu.

    Mfanye mfanyalo lakini kaeni mkujuia damu ya mtu haiendi bure huyo Lulu mpaka atajifungulia magereza na mtoto apimwe DNA kama kweli ni wa Kanumba au wa mibaba mingine.

    ReplyDelete
  20. Hivi hao askari wote ni wa nini?

    ReplyDelete
  21. nadhani watanzania tunaupungufu fulani, leo kwa kuwa Kanumba hayupo tayari msshamsahau mnaanza kumtetea huyu binti angekuwa ni mdogog asingejihusisha na mapenza na Kanumba ambae ni kama kaka yake mkubwa sana. acheni unafiki kisa mmeona tu picha tayari mnajitia mnamuonea huruma. vipi kuhusu familia ya Kanumba,vipi kuhusu kanumba na maisha yake kukatishwa just like that. Huyu Lulu angekuwa si mtu mbaya kwa nini amuache Kanumba akiwa meanguka chini bila hata kujali kujua kama ameumia, at least angepiga kelele watu waje wamsaidie kuwa Kanumba kadondoka na hajui kama amepatwa na shida gani badala yake akaondoka na kumuacha akiwa chini na kuondoka. alafu nyinyi mnakuja hapa na kuanza kusema jamani kadogo wanamuonea blabla kibao. sioni haja ya kuufumbua ukweli macho angalieni hili tatizo katika mbande zote nasi kuona huruma bila kuangalia haki iko wapi. watoto wangapi wanajihusisha na vitendo vya ugaidi na kuua ma million ya watu so kuwa mtoto si hoja na watanzania muache unafiki.

    Mdau sweden

    ReplyDelete
  22. Hatii hata huruma, macho makavu hana wasiwasi anahangaika tu na hiyo hijabu hapo in my opinion

    ReplyDelete
  23. Nimependa sana kivazi cha huyu Lulu!! Kwa kweli anapendeza na ninapendekeza kuwa uvaaji wa aina hii uendelezwe na kuhimizwa.

    ReplyDelete
  24. Tusipende kuhukumu kwa jambo tusililofahamu janga linaweza kumpata yeyote anayejua ukweli ni Mwenyezi Mungu peke yake, kuhusu wakili kujitokeza kumtetea kila mtu na bahati yake. Hivi Lulu ndo angekufa kanumba naye angepewa msukosuko hivi au lulu angekuwa mtoto wa kigogo angepata msukosuko hivi, hivi sasa kanumba marehemu kila mtu anajidai anampenda mbona wakati hai alikuwa na maadui leo hii kila mtu anajidai mwema kwa kanumba, Wabongo tuache unafiki. Sisi tuna hukumu tuna makosa mangapi mbele ya mwenyezi Mungu?

    ReplyDelete
  25. Nimefurahi sana niliposoma habari hii hadi machozi yananitoka kwa furaha kwa jinsi Mawakili walivyojitokeza kumtetea Lulu na jinsi Hakimu anayeshikilia kesi hii kuwa na moyo wa huruma vile vile Maaskari kwa kumlinda Lulu, Inshallah M/Mungu awape nguvu na afya njema hadi mwisho wa kesi hii.

    Inshallah Mwenyenzi Mungu ataleta wepesi kwenye hili na Lulu atakuwa huru kwani kwa mtu muelewa Lulu hana kosa kwa mujibu wa ripoti ya Madaktari bt kisheria hatuna budi kusubiri uamuzi wa Mahakama na nina imani haki itatendeka.

    ReplyDelete
  26. Jamani mnaona vazi la heshima jinsi gani lipo juu je ugepiga mapigo yako ya kujiachia....? jamani vazi la heshima ni zuri na linakubarika sehemu yoyote.

    ReplyDelete
  27. mhh!limetokea lakutokea hata wamfanyeje lulu kanumba kashatutoka,cha msingi sheria ifwate mkondo wake, na lulu amepata fundishola maisha yake yote..mimi namuombea tu Mungu amsamehe tu lulu. atulie ajenge maisha upya. ila am worried wananchi wanahasira sana bado machungu hajaisha ndo kwanza tukimwona lulu tunamkumbuka Kanumba!what is going to happen for her atakapo kua set free...wazazi wake wajipange pa kumpeleka mpaka hai ya hewa itakapotulia..

    ReplyDelete
  28. M/Mungu atashusha rehma zake kama hana kosa basi atamlinda na kama anakosa basi atamhukumu, yeye ndio anaejua nini kilitokezae .

    ReplyDelete
  29. Binafsi simuonei huruma anavuna alichopanda mtoto mdoga kama yeye alitakiwa atulie nyumbani asiye sikia la mkuu huvunjika guu na ngoma ili lia sana mwisho wake hupasuka alikuwa akijigamba kila kukicha me mzuri me mzuri kiko wapi? sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine

    ReplyDelete
  30. hao wanaosema anatia huruma nonsenses au aliyekufa kafa, huyu ndio aliyekuwa nae kanumba kabla ya kifo chake, eti pombe ndo imemuua angekutwa kafa peke yake chumbani kweli lkn alikuwa nae kamsukuma, anatia huruma rahisi tu kusema ee kanumba yuko wapi ss anaoza uko, eti nitampa hifadhi Norway labda usiwe na mume ukiwa na mume masaa 24 kwa escort utamrudisha kwa wizi wa mumeo wangesema kaua bila kukusudia kidogo ningeelewa, mtoto mwenyewe maadili o, halafu hapo kaenda mahakamani amevaa mkufu ivi ukiingizwa lokapu si unavulishwa kila kitu kama cheni, shanga mkanda ss yy vipi usikute hata selo hali hii ndo tanzania yetu sehria f

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...