Nanapenda kuwapa pongezi Watanzania wenzangu waishio Marekani na Mexico tunaposherehekea miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya wenzangu hapa Ubalozini nawatakia Watanzania wote heri na fanaka ya siku hii muhimu katika historia ya nchi yetu.
Aidha, tunaposherehekea sikukuu hii, natoa wito kwa Watanzania wote kuendeleza udugu na mshikamano wetu, ili muungano wetu udumu na taifa la Tanzania lizidi kusonga mbele.
Mwanaidi Sinare Maajar
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico
Washington, DC.
April 25, 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...