mtaalamu wa uwekezaji akitoa mrejesho nyuma juu ya tathimini ya uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania.
 Mkurugenzi mkuu wa SSRA (kushoto) akiongea na mtaalaamu wa maswala ya hifadhi ya jamii kutoka nchini Chile.
 wadau wa sekta ya hifadhi ya Hifadhi ya jamii wakimsikiliza mtaalamu wa uwekezaji.


Katika kusimamia  na kuhakikisha kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii inaendeshwa vyema,kwa manufaa ya wanachama na taifa kwa ujumla, leo hii wadau wa sekta ya Hifadhi ya jamii(wawakilishi wa serikali, vyama vya wafanyakazi, vyama vya waajiri, wakuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii ama wawakilishi wao walikutana katika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini DSM ili kupokea taarifa ya tathimini ya uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii Tanzania,toka kwa Mtaalamu wa Uwekezaji.
Vilevile walipata fursa ya kusikia jinsi mifuko ya Hifadhi ya jamii inavyojiendesha katika bara la Amerika Kusini.
Mkutano huo uliandaliwa na Benki Kuu ikishirikiana na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii(SSRA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...