Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, Zainabu Abbasi pamoja na mwanawe, Kheri Hasifu wakipokea boksi la sabuni ya kufulia kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ilala, Gaudence Shawa katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na pia kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, Lucy Sozigwa.

 Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ilala, Gaudence Shawa (kushoto) akikabidhi msaada wa mashine ya kusaidia mgonjwa kupumua kwa Katibu wa Afya wa Hospitali ya Temeke, Lucy Sozigwa hospitalini hapo, Dar es Salaam leo. Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo wafanyakazi 45 wa NBC wa kanda huyo wakishiriki shughuli za kusafisha mazingira. Katikati ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Sr. Bertha Matiya.
  Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya NBC, Ali Lwano akigawa sabuni kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na pia kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo Dar es Salaam leo.

 Wafanyakazi wa benki ya NBC, Janeth Mutahanamilwa (katikati) na Ammanuel Mseti (kulia kwake) wakigawa sabuni kwa baadhi ya wagonjwa na watoto wao waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, katika tukio ambalo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na pia kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala wakisafisha mazingira ya hospitali hiyo wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wa Kanda ya Ilala na watumishi wa Hospitali ya Temeke wakipozi kwa picha katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vifaa vya tiba na sabuni na pia kushiriki shughuli za usafi hospitalini hapo Dar es Salaam jana. Matawi yaliyoshiriki katika hafla hiyo ni,  hiyo Corporate, Mnazi Mmoja, Kichwele, Samora, Industrial, Kariakoo, Muhimbili, Chang’ombe na Mbagala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...