Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imetoa taarifa usiku huu juu ya ujumbe mfupi wa simu uliokuwa ukisambazwa kwa watumiaji wa simu za mikononi hapa nchini uliokuwa ukieleza kuwa ifikapo saa tano usiku (kwa masaa ya Afrika Mashariki) watumiaji wa simu hizo wanatakiwaa kuzizima simu zao kutokana na mionzi ya Sarari moja ambayo ingepita karibu na Dunia na ambayo inasemekana kutokana na mionzi hiyo watu watumiao simu hizo wangeweza kupoteza maisha au kupatwa na madhara makubwa kama wasingekuwa wamezima simu zao.

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imekanusha vikali taarifa hizo na kusema taarifa hizo ni za uongo na kuifananisha taarifa hii na ile ya miaka kadhaa iliyopita ilikuwa ikisema kuwa kuwa makini na ujumbe mfupi wa mionzi.

TCRA imewataka wananchi woote na watumiaji wa simu za mkononi nchini,kuzipuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zimeanzishwa na mtu ambaye hana lengo zuri kwa watumiaji wa simu za mikononi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. jaman nyie tcra, lisemwalo lipo na kama halipo laja..nyie kila siku ni watu wa kukanusha tu..sasa siku ikija kutokea kuwa yaliyosemwa ni ya kweli na watu wakayapuuza wakiamini kuwa mtakanusha kumbe ni kweli si itakuwa ni maafa?..sisi wengine tuko mbali na bahati mbaya hatupati habari kwa wakati..hii ni hatari sana jamani..kwa mfano mie kama ingekuwa au kama ni kweli mm tayari ningeshapata la kunipata maana taarifa naipata nyuma ya muda..sasa jijengeeni mazoea ya kuweka post zenu kwenye mitanadao ya kijamii kama huu wa michuzi mara kwa mara ili angalau tuwe tunapata taarifa rasmi toka kwenu kwa wakati na si kusubiri mtu aseme na nyie ndo mkanushe..this is a shame for professions like you guys..ukizingatia simu za ajabu ajabu siku hizi zinauzwa kama nyanya sokoni, sio tcra wala tbs wanaozuia hilo, sasa tunajuaje kama zina viwango angalau kidogo vya kuzuia mionzi au ndo mabomu mikononi kwetu?..halafu na sisi walala hoi simu tunzihitaji,kama zimeruhusiwa kuuzwa sisi tunaona zina viwango kumbe sio...hatari

    ahsnte
    hsm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...