Watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na wadau wa Taasisi ya Badef wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja kumalizia maandamano yao yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo,maandamano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Badef kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia albino nchini.

Na Mwandishi Wetu

Shilingi milioni mbili zimekusanywa katika Harambee ya kusaidia kampeni ya kufanikisha maendeleo ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini iliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Waliochangia fedha hizo ni Waziri wa Afya na Usatwi wa Jamii Mh.Dkt. Hadji Mponda aliyetoa milioni moja,Meya wa Manispaa Kinondoni Ndg.Yusuph Mwenda alitoa laki tano huku Mbunge wa Viti Maalum Mh.Shaimaar Kwegyr akitoa laki tano.

Akizungumza na watu waliojitokeza katika matembezi hayo Mwenyekiti wa Taasisi inajishughulisha na maendeleo ya watu wenye ulemavu iitwayo Badef, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mh.Salum Barwany ambae Mbunge wa Lindi Mjini alisema kuwa shilingi milioni 500 zinahitajika.

Mh.Barwany alisema kuwa walemavu wa ngozi wanakabiliwa na tatizo la kansa ya ngozi ambayo inawashika kiurahisi zaidi kutokana na ngozi yao hivyo fedha hizo zitasaidia kuwanunulia mahitaji muhimu watu hao.

Alisema kuwa pia wanakabiliwa na tatizo la elimu kwa kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana tatizo la kuona mbali hali inayowafanya kushindwa kuona vema darasani hivyo wanahitaji msaada maalum.

Alisema kuwa hizo ni moja kati ya changamoto ambazo jamii inatakiwa kuwasaidia walemavu hao kukabiliana nazo ambapo ili kufanikisha hilo kuna haja ya kufanya utafiti.

Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kufanya utafiti wa kubaini namna ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi katika nyanja za elimu, kijamii na hata uchumi.

Pia Mh.Barwany alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuwasafirisha kiurahisi albino ambao watakuwa na dalili za kansa ya ngozi ili kuwahi katika hospitali za rufaa kwa ajili ya matibabu.

“ Kwa sasa sisi walemavu wa ngozi tunahitaji milioni 500 ili angalu tuweze kusimamia na kujipatia mahitaji yetu muhimu ya kiafya hapa nchini, hivyo wanajamii tunaomba tusaidiane katika hilo tafadhali” alisema Barwany.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alitakiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh.Dkt.Hadji Mponda ambae hakuwepo na hivyo aliwakilishwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda.

Maandamano yalianzia Viwanja vya Leaders na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja.

Vilevile unaweza kuchangia kupitia: Mpesa Namba; 0769696999, Airtel Money Namba; 0688858535, TigoPesaNamba; 0655029595 au kwenye akaunti ya BADEF (CRDB Bank, Lumumba Branch Akaunti Na. 0150278228900).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nani awape FURSA??? FURSA zipo zitafuteni wenyewe? Mpaka muonewe huruma????

    ReplyDelete
  2. kwa kweli lile bango lenye maneno "albino sisi ndugu zenu tupendene"
    naomba kaka uweke website ya ndugu zetu hawa kwenye hii blogu ili ndugu wengine waweze kutembelea na kusaidia nami ni kichukua fursa kuwaimiza watanzania wengine popote walipo tuwasaidieni ndugu zetu hawa kwani kutoa ni moyo na msaada auishii kwenye familia yako tu bali pia kwa watu wengine usiowajua.

    ReplyDelete
  3. ndugu zangu albino tuko pamoja na nyie ila niwang'ate sikio kuna fursa mnayo ya kukimbilia nchi yeyote ya ulaya pia hapa marekani,nendeni kwenye balozi za nchi husika mkachukue viza zenu zinawasubiri na mkifike huko mnapewa hadhi ya ukimbizi haraka sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...