Kwa watanzania pamoja na marafiki!

Kamati ya muda iliyoteuliwa Ubalozini kwa nia ya kuanzisha chama cha watanzania Sweden inawakaribisha katika hafla fupi ya ufunguzi wa chama na pia kuchagua viongozi watakaondeleza shuguli za chama.

Mgeni wa heshima katika ufunguzi na uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Watanzania atakuwa Mh. Balozi Muhammed Mwinyi Haji Mzale.

Sehemu: Tanzania house, Näsby Allè 6, Täby
Wakati: Saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni.

Mwaliko utatumwa kwa barua pepe ikiambatanisha fomu za kujiandikisha kugombea uongozi wa chama. Pia waweza kupakua katika tangazo lilowekwa katika tandao wa Ubalozi.

Wote mna karibishwa na Ukipata taarifa hii tafadhali mtumie na mwingine!

Kamati ya wanamchakato kupitia


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kumradhi wakuu, mimi nina swali kuhusu hili suala.

    Tangazo linasema kuanzishwa kwa "Chama".

    Swali langu ni: hii huwa ni Chama ama Jumuiya?


    Nisaidieni kuelewa waungwana.

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni hapo juu nipo pamoja na wewe kabisa. Mimi nadhani waseme Jumuiya. Maana Jumuiya unakuwa mshiriki pale unapokuwa nchi husika lakini ukiondoka ushiriki unakoma. Na jumuiya huwa na mchango mdogo mdogo kwa ajili ya kusaidiana ktk majanga mbalimbali. Pia jumuiya inakuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara ili kuweza kupokea wanajumuiya wapya, vilevile pamoja na ku-interact. Lakini mikusanyiko hiyo haiutumia pesa ya wanajumuiya iliyokwisha kuchangwa awali. Bali kila mwanajumuiya hutoa mchango kuwezesha mkusanyiko. Lakini pia mkusanyiko huo waweza kufadhiliwa na mfadhili kama akipatikana ndani ya jumuiya au nje.

    Lakini kama ni CHAMA, hiki ni lazima kiwe na OFISI za kudumu. Na mwanachama hakomi kuwa mwanachama, maana atakuwa ameweka hisa zake. Ikitokea mwanachama mwenyewe akafa, pia uanachama haukomi, inabidi mrithi achukue nafasi. Pia CHAMA kinakuwa na malengo ya KIUCHUMI, ambayo mara nyingi melengo hayo ufahamika kwa waanzilishi zaidi ya wanachama wa kawaida (ordinary members). Kwa kifupi AGENDA ya CHAMA huwa ni SIRI ya WAANZILISHI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...