Wazee ndiyo chimbuko letu..mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya NHIF pia ni Rais wa CWT Bwn. Gratian Mukoba akitoa msaada wa mashuka kwa wazee waliopo kwenye kambi ya wazee ya kolandoto,ikiwa ni katika mwendelezo wa siku ya wadau wa NHIF mkoani Shiynyanga.
Pokeeni msaada huu ili uwasaidie wahitaji hususani akina mama wajawazito walale sehemu safi na watoto watakaojifungua.
Hata wodini tunafanya kazi ....ni mjumbe wa bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya Bwn. Gratian Mukoba akimsikiliza  mwalimu Devotha Msenyu aliyekuwa amelazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa matibabu wakati wa kutoa msaada wa mashuka kupitia siku ya wadau wa NHIF mkoani humo.
Watoto wanayofuraha punde wanapomuona mama akimjali kulia ni Bi christina Ilumba mwanasheria wa NHIF akimfunika mtoto Hasma masanja kwa shuka likiwa ni sehemu ya msaada kwenye wodi ya watoto ya hospitali ya kolandoto.

NHIF inayo dhamira ya dhati katika kusaidia makundi maalum hususani wazee kupitia mipango yake mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya,pichani ni Mjumbe wa bodi,waganga wafawidhi wa mkoa na kambi ya wazee,watumishi wa mfuko wa kanda na makao makuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CHF ni nini na NHIF ni nini maana naona mnanichanganya na nina uhakika siko penge yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...