Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Katanga katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Petro Masumbuko(37), amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi mbavuni na majambazi kisha kupora shilingi elfu saba na simu moja ya mkononi.

Kamanda wa Polisi mkoni Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana marija ya saa 2.00 usiku baada ya kundi la watu wenye silaha kumvamia Bw. Masumbuko nyumbani kwake na kumpiga risasi kabla ya kumpora fedha hizo pamoja na simu yake ya mkononi aina ya Nokia.

Kamanda Kashai amesema majeruhi amekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya pamoja na matibabu huku Polisi nao wakiendelea na uchunguzi na kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.

Wakati huo huo, Polisi mkoani Kigoma wameanza uchunguzi wa kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Kazegunga kilichopo katika kata ya Msimba Bw. Riziki Issa Mahela(32), aliyekutwa huko kwenye eneo la Kahabwa mjini Kigoma akiwa ameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga kichwani na mgongoni.

Kamanda Kashai, amesema kuwa Polisi watatafuta chanzo na sababu za mauaji hayo na kitu kilichomfanya marehemu asafiri kutoka katika eneo la kijijini kwake hadi katika mtaa huo ambako ameuawa.

Huyo ni mtu wa tato kuuawa katika mazingira ya kutia mashaka katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo watu wengione wane waliuawa katika matukio matatu tofauti huku wawili mtu na mkewe wakiuawa kwa tuhuma za imani za kshiirikina.

Kamanda Kashai amewaonya vikali wale wote wenye kuchukua sheria mkononi kwa kuwazuru hata kuwaua wengine kwa sababu zozote zile kuwa watapambana na mkono wa dola kwa vyovoyte iwavyo.

Amesema Makachero wake wamejipanga kuhakikisha kuwa kila mtu aliyehusika katika mauaji ya mmoja wa marehemu hao kuwa ni lazima akamatwe na sheria kuchukua mkondo wake.

Amewataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo li kusaidia kufanikisha kukamatwa wa washukiwa wote wa mauaji hayo.

Taarifa hii imehaririwa na kusambazwa kwenu na Inspekta Mohammed Mhina, Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Ndugu Mhina, kwa nafasi yako kama afisa habari Mkuu wa jeshi nakushauri utafute msaada wa ''language therapy'' ili uweze kuhariri vizuri taarifa kama hizi: jana marija ya saa 2....mtu wa tato, watu wengione, imani za kshiirikina ....its too much kwa taarifa moja tu.

    Mdau!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2012

    Anon. wa mwanzo hapo juu afadhali umeliona hilo mwenzangu, mana hata hicho kichwa cha khabari naona kina 'mushkel' kidogo, badala ya kuandika "SHILINGI..." kimeandikwa SHILIMGI... Mtu unasoma khabari mpaka unachefukwa kwa makosa madogo madogo ya kizembe tu, nae huwa mnaharakia nini kuzipachika humu badala ya kukaa kwa kituo kuzihariri ndio mkaziweka, mnafanya mashindano kwani kuona nani ataweka khabari yake mwanzo humu au kulikoni? Aaaa! hebu kuweni makini na kazi zenu na siyo kuripuwa ripuwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2012

    TShs. 7,000/= zinamjeruhi mtu.

    Ujambazi sasa basi!

    Ni bora kwenda kulima maana miaka ya kuchuma imekwisha sasa, watu wamefilisika mifukoni ni vigumu kwa maisha haya kumkuta mtu anatembea na bunda la pesa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2012

    Maisha yamekua magumu Tanzania, hiyo shilingi elfu saba ni ya kunulia pipi huku nchi za watu, Au ni nauli ya kwenda na kurudi kwa daladala!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...