WIKI moja baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kupata ndege aina ya Boeing 737-500 iliyoanza rasmi safari za Dar es Salaam-Kilimaanjaro-Mwanza wikendi hii, Shirika hilo limeanza mchakato utakaoliwezesha kupata ndege nyingine kati ya wiki tatu au sita zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya safari hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL,Paul Chizi alisema shirika lake linatarajia kupata ndege nyingine aina ya Boeing ambayo italiwezesha shirika hilo kufanya safari za nje zikiwemo Dar es Salaam-Lusaka, Dar es Salaam-Harare na baadae Dar es Salaam-Dubai.

“Tumeanza utekelezaji wa mpango kazi wetu wa muda mrefu ambao utatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.Katika mpango wetu ,tunatarajia kupata ndege nyingi na bora zaidi. Kwa kuanzia,tunatarajia kupata ndege nyingine katika kipindi cha wiki tatu mpaka sita na ndege hiyo itatuwezesha kuanza safari za kimataifa." alisema Chizi.

Chizi aliwataka wananchi pamoja na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za Shirika lake na kuahidi kuwa shirika hilo litazingatia utoaji wa huduma bora kwa bei nafuu. “Mafanikio ya shirika yatategemea mchango wa wadau mbali mbali. Tunaomba wananchi watuunge mkono ilituweze kupata mafanikio zaidi,” alisema.

aliendelea kusema kuwa katika wiki chache zilizopita kampuni yake ilizindua tovuti ambayo itasaidia katika kuboresha huduma ya ukataji tiketi kwa wateja kwa wakati wao na kuboresha utoaji huduma wa kampuni.

“Kitu cha kujivunia ni kuwa wateja sasa wanaweza kutaka tiketi kupitia mtandao bila kufika katika ofisi zetu au kupitia mawakala wetu kama ilivyokuwa zamani,” alisema.

Nae Jaji Mstafu wa Mahakama Kuu ambaye alipata nafasi ya kusafiri kwa kutumia ndege mpya ya shirika hilo aliomba Serikali kutoa ruzuku kwa Shirika hilo na kusisitiza kuwa uboreshaji wa shirika hilo utaongeza pato la taifa kupitia sekta ya Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2012

    BRAAVOOOOOOO ATCL...Hao wanaolihujumu shirika letu tulipendalo tukiwabaini ni 'itakuwa halali yetu'.Wakimùbize hao mafisadi na sahauni yaliyopita.Blog ya jamii naomba mnifikishie ujumbe huu kwa ATCL..

    Uniform za hao wahudumu wanaonaje rangi ikawa ya kibluubluu kuendana na rangi ya ndege badala ya hii brown..ingependeza sana.

    Hii ndege 737-500 haina rangi ya bluu kwenye engine zake na kule mkiani(Kama hiyo picha ya zamani)..Rangi bluu kwenye engine na mkiani,na twiga zinapendeza sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2012

    hehehheeh uwiii jamani majina mengine yana raha kweli nanukuu (chizi aliwataka watu waunge mkono jitihada za shirika lake ) mwisho wa kunukuuu .. hehehehe uwiiii mabu zangu asante michuzi

    ReplyDelete
  3. Rasul NgomaMay 21, 2012

    I would like to Congratualte Mr. Chizi on the way he is changing Air Tanzania around. i think his expertise and experiance should have been appreciated long before, Air Tanzania could not be where it is now. I appeal to the goverment of Tanzania through the great leadership of his excellence Ndugu Jakaya Kikwete to put weight behind our Airline, help it acquire more planes which we seriously need to put a mark in the aviation industry and put Tanzania where it belong in the African Continent. Mr. Chizi please when you get more planes please revive the Dar/ Mahe/ morono/Dar route. I worked in Seychelles before and i know how many tourists wants to come to Tanzania and for sure Kenya airways is coining on that big time(just a suggestion). Finally i cant express my joy to see that Our airline is finally moving to a right direction.

    Thank you,

    Rasul Ngoma
    Food and Beverage Manager,
    Crown Plaza Hotel Nairobi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...