Basi la abiria la kampuni ya NBS lenye nambari za usajiri T978ATM aina ya Scania,leo limepata ajali mbaya maeneo ya Jineri kilomita kadhaa kabla ya kufika kwenye mji wa Igunga Mjini Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo.Waliopoteza Maisha ni wanaume watatu na wanawake watatu pamoja na mtoto mmoja wa kiume ambao wote majina yao hayakuweza patikana mara moja. Basi hilo lilikuwa linatokea mkoani Tabora kuelekea Jijini Arusha. (PICHA NA MDAU ABDALLAH AMIR,TABORA.)
Home
Unlabelled
basi la NBS lapata ajali leo mkoani Tabora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Sad news indeed, poleni kwa wafiwa, Mwenyezi Mungu awapumzishe marehemu pema peopeni Amen, na waliojeruhiwa wapate nafuu haraka.
ReplyDeleteJamani! poleni sana waathiriwa wa tukio hili. hatujui chanz cha ajali lakini pengine ni yale yale ya speed na uendeshaji mbaya. Wanchi tuwe askari wenyewe. Kama dereva anaendesha rafu pigeni kelele mshuke! maana hata mkipigia simu polisi watapeana rushwa kiishe! Watu watajiwe jina la Kampuni ili waepuke kupanda magari kama haya.
ReplyDeletePOLENI SANA WAFIWA, MAJERUHI TUNAWAOMBEA MPATE NAFUU HARAKA.
ReplyDeleteHaya mabasi ya NBC na mengine pia huenda speed mno nyakati za usiku kwa vile watu wa usalama mida hiyo huwa hawapo barabarani.
Yaliwahi kunipita speed nikiwa na gari ndogo maeneo ya Ziba- Igunga njia ya kuelekea Ndala yakiwa speed usiku, wakati barabara ikiwa mbaya. Yaani, niliyakuta Tabora yameshapark.
Lakini, kuna jambo hili inabidi nalo liangaliwe, Matajiri wengi wenye mabasi huku bongo wanafanya biashara kwa KUTOA KAFARA. Kwanza, utakuta hawaendelei wengi maisha yao hovyohovyo; pili, wengi ukishaona ajali zinakuwa nyingi baada ya muda ANATOA MABASI MAPYA. Na wengi wao utakuta either wamewafanya WATOTO wao au ndugu MANDONDOCHA. NYIE WAFANYA BIASHARA ACHENI BIASHARA ZENYE IMANI YA UCHAWI.
TUMWOMBE MWENYEZI MUNGU ILI WENYE BIASHARA ZA UCHAWI WASHINDWE KUFANYA BIASHARA HII TENA.
mhmmm nashukuru mungu mdogo wangu amefika salamaa maana ameenda tabora majuzi na magari ya cmpuny hiyo mbn ingekuwa hekaheka sasa hv poleni sn wafiwa
ReplyDelete