Basi la abiria la kampuni ya NBS lenye nambari za usajiri T978ATM aina ya Scania,leo limepata ajali mbaya maeneo ya Jineri kilomita kadhaa kabla ya kufika kwenye mji wa Igunga Mjini Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo.Waliopoteza Maisha ni wanaume watatu na wanawake watatu pamoja na mtoto mmoja wa kiume ambao wote majina yao hayakuweza patikana mara moja. Basi hilo lilikuwa linatokea mkoani Tabora kuelekea Jijini Arusha. (PICHA NA MDAU ABDALLAH AMIR,TABORA.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2012

    Sad news indeed, poleni kwa wafiwa, Mwenyezi Mungu awapumzishe marehemu pema peopeni Amen, na waliojeruhiwa wapate nafuu haraka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    Jamani! poleni sana waathiriwa wa tukio hili. hatujui chanz cha ajali lakini pengine ni yale yale ya speed na uendeshaji mbaya. Wanchi tuwe askari wenyewe. Kama dereva anaendesha rafu pigeni kelele mshuke! maana hata mkipigia simu polisi watapeana rushwa kiishe! Watu watajiwe jina la Kampuni ili waepuke kupanda magari kama haya.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2012

    POLENI SANA WAFIWA, MAJERUHI TUNAWAOMBEA MPATE NAFUU HARAKA.

    Haya mabasi ya NBC na mengine pia huenda speed mno nyakati za usiku kwa vile watu wa usalama mida hiyo huwa hawapo barabarani.

    Yaliwahi kunipita speed nikiwa na gari ndogo maeneo ya Ziba- Igunga njia ya kuelekea Ndala yakiwa speed usiku, wakati barabara ikiwa mbaya. Yaani, niliyakuta Tabora yameshapark.

    Lakini, kuna jambo hili inabidi nalo liangaliwe, Matajiri wengi wenye mabasi huku bongo wanafanya biashara kwa KUTOA KAFARA. Kwanza, utakuta hawaendelei wengi maisha yao hovyohovyo; pili, wengi ukishaona ajali zinakuwa nyingi baada ya muda ANATOA MABASI MAPYA. Na wengi wao utakuta either wamewafanya WATOTO wao au ndugu MANDONDOCHA. NYIE WAFANYA BIASHARA ACHENI BIASHARA ZENYE IMANI YA UCHAWI.

    TUMWOMBE MWENYEZI MUNGU ILI WENYE BIASHARA ZA UCHAWI WASHINDWE KUFANYA BIASHARA HII TENA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2012

    mhmmm nashukuru mungu mdogo wangu amefika salamaa maana ameenda tabora majuzi na magari ya cmpuny hiyo mbn ingekuwa hekaheka sasa hv poleni sn wafiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...