Rais wa zamani wa Liberia, Charles taylor, amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikiendeshwa dhidi yake ya kuhusika na uhalifu wa kivita.

Mwezi uliopita, mtawala huyo wa zamani wa Liberia, alikutwa na hatia ya kuhusika katika kuviwezesha vikundi vya kigaidi nchini Sierra Leone, na mahakama maalum nchini Sierra Leone, kupitia kwa jaji wake mmoja imeeleza kuwa hukumu hiyo imeendana na kiwango cha makosa aliyoyatenda Bw. Taylor.

Taylor mwenyewe kwa upande wake ameendelea kusisitiza kuwa hakuhusika na tuhuma zilizopelekea kuhukumiwa kifungo hicho na taarifa za awali zinaeleza kuwa anatarajiwa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo. Mchakato wa kukata rufaa hiyo unaweza kuchukua hadi miezi sita.

Alikuwepo mahakamani wakati hukumu dhidi yake ilipokuwa inasomwa, na hakuonekana kushtushwa na lolote lile zaidi ya kutulia mahali pake alipokuwa amekaa huku akiwa amevalia nadhifu kabisa suti yake na tai maridadi.

“Mtuhumiwa amekutwa na hatia ya kuhusika katika kuviwezesha vikundi vya kigaidi katika matukio mabaya kabisa ya kigaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia hii” alisikika jaji Richard Lussick akitamka wakati wa usomwaji wa hukumu hiyo ambayo imekuja baada ya miaka takriban mitano ya usikilizwaji wa shauri lenyewe.Kwa habari zaidi Bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2012

    Hii ndio nchi yenye utawala wa sheria sio Tanzania ambapo kila mmoja ana sheria inayomhusu peke yake, kama wewe ni mwenzangu na mimi sheria fulani inakufunga, kama wewe ni mwenzao na wale, basi sheria inatumika nyingine ya ki-hao hao

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2012

    Charles Taylor,

    Hii Hukumu ina maana ni kuwa ni zaidi ya miaka 10 iliyopita (tokea 30 May,2002) alishafariki Dunia yupo Kaburini wakati hukumu ilipotoka jana.

    Wastani wa kuishi Duniani ktk nchi nyingi ni chini ya miaka 100 (Life expectance.

    Yeye ana umri wa miaka 60+ Hivyo basi:

    Thus 60+50=110
    Then 110-100=10+

    Charles Taylor alishafariki Kabla ya 30 May 2002 !!!

    Mpo hapo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2012

    Unadhani angehukumiwa kwao angelamba miaka hiyo. Angekutwa hana hatia. Hayo ni mambo ya The Hague. Viongozi wa nchi zinazobeba viongozi wavunja sheria watie akili. Majaji the Hague wanawasubiri kwa hamu. Hii mahakama naipendajeeeee!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2012

    Nakubaliana kabisa na mdau wa hapo juu. Bongo sheria zetu zinatofautiana na madaraja. Nyie ngojeni mwisho wa kesi ya Kanumba...Sisemi mengi..Michuzi naomba usinibanie hii. Mkereketwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...