Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini kuhusiana na Vurugu Zilizotokezea Zanzibar,hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.
Baadhi ya Mawaziri waliohudhuria katika Mkutano wa Rais na Vyombo vya Habari mbalimbali akielezea vurugu zilizotokezea Zanzibar na hatua zilizochukuliwa na Serikali na kuchukuliwa hatuwa wale wote waliohusika na vurugu.hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.
Mwandishi wa Habari Farouk Karim akiuliza maswali katika Mkutano wa Rais na Vyombo vya Habari mbalimbali akielezea vurugu zilizotokezea Zanzibar na hatua zilizochukuliwa na Serikali na kuchukuliwa hatuwa wale wote waliohusika na vurugu.hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi
Mwandishi wa Habari Mwantanga Ame wa Gaazeti la Zanzibar leo akiuliza maswali katika Mkutano wa Rais na Vyombo vya Habari mbalimbali akielezea vurugu zilizotokezea Zanzibar na hatua zilizochukuliwa na Serikali na kuchukuliwa hatuwa wale wote waliohusika na vurugu.hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar leo,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote,atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”

Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya uvumilivu wa kidini.

“Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema Rais Dk. Shein.

Alisema ameshangazwa na vitendo vya uchomaji makanisa moto vilivyofanywa wiki iliyopita akihoji kwamba kulikuwa na uhusiano gani baina ya Muungano na makanisa “Mie nilikuwa nashangaa sana hivi kuna uhusiano gani kuzungumzia Muungano na kuchoma makanisa,kupora mali za watu” Alisema Dk. Shein.

Rais Dk. Shein alisema matatizo ya Muungano yanashughulikiwa chini ya utaratibu uliokubaliwa na Serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna kamati ya kushughulikia kero za Muungano na hadi sas kuna mambo 12 yanafanyiwa kazi ikiwemo suala la mafuta na gesi asilia.

“Taratibu za kutatua kero za Muungano zinaendelea, kuna mambo 12 yamewasilishwa katika kamati na yanafanyiwa kazi, miongoni mwa hilo ni suala la mafuta na gesi asilia, sisi tumeshaamua, SMT bado haijaamua ,lakini sisi tumeamua kuyaondoa katika Muungano, lakini nasema ndugu wawili hawagombani…tutakubaliana” Alisema Rais Dk. Shein.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao na akielezea kuw ahiyo ni fursa muhimu kwa Wazanzibari kueleza wanataka katiba iweje na kuwatoa wasiwasi kuwa hakuna atakayetishwa na wasiogope,lakini akasisitiza ni lazima wasubiri Tume ndipo watoe maoni yao maana wakieleza sasa hakuna anayawasikiliza.

“Wanaotoa maoni yao kuhusu Muungano kwa hivi sasa wanapoteza muda wao, ni sawa na kusema na ukuta tu kwani hakuna anayewasilikiza, hakuna anayechukuwa maoni yao maana Tume haijaanza kazi,wasubiri itakapoanza wakatoe maoni yao” Alisema Rais Dk. Shein.

Rais Dk Shein alitoa ufafanuzi huo akijibu swali la waandishi waliohoji kuwepo kwa kamati ya kutatua kero za Muungano na mjadala wa katiba mpya kwamba Serikali ingesubiri matokeo ya Tume ya Katiba kuhusu Muungano maana inawezekana mambo yakabadilika.

“Sheria ya Tume ipo wazi, lazima wafuate sheria na taratibu hatazuiwa mtu kutoa maelezo yake,lakini kero za Muungano zinaendelea kushughulikiwa kuwepo kwa Tume ya Katiba hakuzuii kamati iliyo chini ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kushughulikia kero za Muungano.

Katika hatua nyengine, Rais Dk. Shein ameipongeza Polisi kwa busara na hatua walizochukua kushughulikia vurugu zilizotokea wiki iliyopita Visiwani Zanzibar ” Nilipopigiwa simu nikauliza kuna alijeumizwa,vifo nikaambiwa hakuna nikasema Alhamdulillah salama” Alisema Dk Shein.

Alisema kwamba licha ya Polisi kuchokozwa na vijana waliokuwa wakichoma moto matairi ya magari barabarani, kuweka mawe na magogo kuziba njia,lakini Polisi ambao walikuwa na silaha hawakutumia silaha hizo,zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi.

”Jeshi la Polisi halibebi lawama,linastahili sifa na kupongezwa…Polisi wana busara sana wanafanya kazi vizuri hawa ndugu zetu wa Polisi kwa kweli lazima tuwapongeze” Alisisitiza Rais Dk. Shein wakati akijibu swali kwamba Polisi wanastahili kulaumiwa, Rais alisisitiza kuwa Polisi walitimiza wajibu wao kwa uzalendo mkubwa wa kuepusha madhara kwa jamii.

”Mimi nilikuwa natoka mazikoni, nilipita barabara ya amani,mwanakwerekwe, nimejionea namna vijana walivyoweka mawe,magogo, kuchoma matairi,lakini Polisi hawakutumia nguvu zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabonu ya machozi, tuwapongezeni Polisi wetu wamejitahidi sana” Aliongeza.

Rais Dk Shein alisema kwa wale wote waliokamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,haki itatendeka kwa kila mtu na kwamba hakuna atayakeonewa wala kudhulumiwa. Pia alisema Serikali inafanya tathimini kuweza kuelewa athari za matukio yaliyotokea. Pia alitumia fursa hiyo kuwapa pole wale wote waliopatwa na matatizo ya vurugu zilizotokea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    msitudanganye, wazanzibar mnachuki na si hivyo tu waislamu mnachuki hata michuzi naye yupo kwani sisi wakristo tukituma maoni kuhusu waislamu haweki ila muisalamu akituma kumkashfu mkristo michuzi anaweka. Makanisa yana uhusiano gani na serikali? Tena Rais wa Tz ni muislamu but because hiyo ni chuki ambayo imeanzia kwenye misikiti yenu na si serikalini. So subirini tu siku s nyingi mtaona maana ni mbegu mmeiotesha matunda yapo soon

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2012

    Safi sana mweshimiwa mzee sheni hotuba imetulia ni ya haki na haija elemea upade wowote.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    Wananchi wa Zanzibar.

    Ni muhimu waelewe hivi:

    1.Ugumu wa maisha hautokani na uzembe wa Serikali pekee, wajiangalie na wao wenyewe mfano tabia ya Umwinyi na kuchagua kazi inaweza kuleta ongezeko la ugumu wa maisha pia.

    2.Ni vigumu ktk Sayari hii kuishi kama upo ndani ya chupa bila kuchanganyika na mtu wa Itikadi nyingine au asili nyingine.

    Mfano nchi za Kikristo za Ulaya kuwa na Wakazi au Raia Waislamu, vivyo hivyo Nchi za Kiislamu kuwa na Wakazi au Raia wa Kikristo.

    3.Wazanzibari msijenge mtazamo potofu kuwa Bara ni Ukristo na Zanzibari ni Uislamu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2012

    Binafsi Dk Shein Namkubali sana.Anajiamini na anajua anaongea nini...Pia yy anaongea na waandishi live ana kwa ana maswali papo kwa papo sio kama huyu mwingine kupitia TV halafu anasoma na hakuna kuulizwa swali...Inaniboa sana.Big up Dk Shein.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2012

    nyie wazanzibari ni watu wa ajabu sana,jitengei halafu muungane na somalia makaninsa ndiyo muungano au mumelaaniwa? unganeni na somalia ili mfaidi sehemu ya bahari kwa kuteka meli na kuua binadamu wenzenu wasio na hatia ndiyo maaana mkapa aliwatia adabu

    ReplyDelete
  6. kibelesecJune 01, 2012

    WAZANZIBAR SI WAVIVU NA NI WASOMI SANA HATA KUSHINDA.......LAKINI TATIZO NI HISIA ZA KIKOLONI ZILIZOJENGWA WAASISI NDIYOMAANA WANATAKA KUJIKOMBOA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2012

    Wafanya fujo Zanzibar:

    Mambo mengine mnayotakiwa kujifunza (inaonyesha mmesahau inafaa mkumbuke)ni:

    1.UHURU:
    Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa Mwingereza tangu tarehe 9 Disemba ,1961.

    2.MAPINDUZI:
    Zanzibar ilisha mpindua Sultani Mwarabu wa Omani tarehe 12 Januari, 1964.

    3.MUUNGANO:
    Zanzibar na Tanganyika zikaungana tarehe 26 Aprili, 1964

    WACHENI NDOTO ZA MWENDAWAZIMU!

    SASA SIO KAZI RAHISI KUURUDISHA UKOLONI WA MWARABU VISIWANI KWA NJIA YA KUUVUNJA MUUNGANO!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2012

    Wapinga Mapinduzi na Muungano:

    WANAPOTAKA KUJIKOMBOA WANAJIKOMBOA KTUOKA KWA NANI NA MARA YA NGAPI?

    WAKATI MWARABU MKOLONI ALISHAANGUSHWA NA MWINGEREZA ALISHATOA UHURU BARA?

    Mulelewe hakuna UHURU juu ya UHURU, wala MAPINDUZI juu ya MAPINDUZI:

    HUO NDIO UBWEGE WA SINTO FAHAMU ZA WAZANZIBAR WAKOROFI WANAODAI WAMESOMA HUKU WAKIWA HAWAJAELIMIKA!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2012

    Mdau

    Fri Jun 01, 11:28:00 AM 2012

    ....WANATAKA KUJIKOMBOA.

    KUJIKOMBOA KWA NANI TENA???

    WAKATI WALIKWISHA JIKOMBOA TAYARI MWAKA 1964 KWA KUMPINDUA MWARABU WAKATOKA KTK MAKUCHA YA MKOLONI WA KIARABU?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 01, 2012

    michuzi uko muugwana sana ndugu yangu ubarikiwe daima amin, yani wanakuambia huwawekei commen zao wakati kila leo commenz zao ndo zinazo tamba na pia matangazo yao ya vilevi(pombe) nakuambia wee acha tu SHUKRAN YA PUNDA MATEKE.

    ETI TUNA CHUKI NAO, SIO WAO WANACHUKI NA SISI HATA HAWATAKI TUPUMUWE NA INGEKUWA SI MUNGU WANGETUZIBA HATA KAULI NA KUPUMUA.

    TUPENI NCHI YETU KAMA MNAONA TUNA CHUKI NA NYINYI CHUKI ITAKWISHA.

    WEWE RAIS KUWA MUISLAM HAJALISHI HIYO KWANI YEYE PEKE YAKE NDO ANAIENDESHA NCHI JEKI WALIO CHINI YAKE NI WA KINA NANI NA WA DINI GANI NA TENA YEYE ANABURUZWA TU OVYOO? WACHA UBU BUBU WEWE

    HUJUI NINI KWAMBA MAKANISA NA SERIKALI YANASHIRIKIANA HUJUI HATA WIMBO WA TAIFA UMETUGWA NA MUIJILISI NA WA KIDINI NA KUFUNGUA BUNGE TUNAUIBA HALAFU TUNAJIDAI NCHI HII HAINA DINI WEWE

    HATUJALALA WALA HATUJASINZIA TUKO MACHO MAPEVU MAKAVU

    TUPENI NCHI YETU TUNAITAKA HATA KAMA HATUIPATI HII LEO ONE DAY TUTAIPA UZIA UISHEEE

    canada

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2012

    Ni jambo zuri Wazanzibari mkapewa nchi yenu, lakini mtegemee mashariti mapya juu ya vitu vyetu kama mtataka na kama vipi mnaweza kuelekea kwa Mtawala wenu wa Ukoloni Mwarabu wa Omani

    Sio mvunje Muungano na sisi halafu mtegemee kuneemeka (kwa baadhi ya vitu) na sisi hiyo haitakuwepo!!!

    HATA SISI BARA TUNGEPENDA MUUNGANO UISHE ILI KILA MTU AENDELEE KIMPANGO WAKE!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 02, 2012

    .......SHUKRANI YA PUNDA MATEKE ???

    Ninyi ndio wenye shukrani ya Punda!

    Angalieni, mna import hadi nyanya, vitunguu na pilipili hoho kutokea Bara kuingiza Zanzibar?

    Hivi mnashindwa kulima wenyewe ktk ardhi yenu vitu vidogo sana kama mboga?

    Hata ukosefu wa nyanya, vitunguu, pilipili na kabechi Visiwani mtadai ni kero na matatizo yanayoletwa na Muungano?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...