Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipofika katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana, kufunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
Baadhi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiondoka katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana,baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    Huu ni ufujaji wa hela za wananchi tu, kwanza hela zimepatikana wapi wakati hazikupitishwa kwenye bajeti ya 2011/2012? Hawa viongozi walipewa semina mara tu baada ya uchaguzi lakini hakuna mabadiliko yeyote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...