WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda, amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege (pichani), kwa tuhuma za ubadhirifu.

Kusimamishwa kazi kwa Ekerege kumekuja baada ya kuwepo sintofahamu ya muda mrefu kuhusiana na kukabiliwa na tuhuma nzito za upotevu wa takriban sh bilioni 38 zinazotokana na ukaguzi wa magari nje ya nchi.

Kigoda alitangaza uamuzi huo jana, na kudai kuwa ni kwa ajili ya kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya tuhuma hizo, ambapo ameunda kamati maalum ya uchunguzi. Hata hivyo, waziri huyo hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na suala la mtendaji huyo mkuu wa TBS.
Waziri huyo aliyeanza kazi wiki iliyopita, alisema ameamua kumsimamisha kazi Ekerege ili kulifanya shirika hilo lirudi katika hali yake ya kawaida ikiwemo kupisha bodi iliyoundwa kutimiza wajibu wake.

Tuhuma dhidi ya Ekerege ziliibuliwa na kamati mbili za kudumu za bunge, ya Mashirika ya Umma (POAC) na Hesabu za Serikali (PAC), ambapo wajumbe wa kamati hizo waliokwenda kufanya ukaguzi nje ya nchi walibaini madudu mengi, ikiwemo kutokuwepo kwa ofisi za ukaguzi kama ilivyodaiwa na shirika hilo, kiasi cha kusababisha upotevu wa sh bilioni 38.
Wajumbe wa kamati hizo walibaini malipo ya kampuni hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi.

Hatua ya kumsimamisha Ekerege, imekuja baada ya mtangulizi wake, Waziri Cyril Chami, kushindwa kumchukulia hatua ikiwemo kumsimamisha, jambo ambalo pamoja na tuhuma nyingine dhidi ya mawaziri kadhaa, lilizua mzozo mkubwa bungeni kiasi cha kuwalazimisha wabunge kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Chami pia inadaiwa alikataa ushauri wa aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyarandu, ambaye alitaka asimamishwe kazi kupisha uchunguzi, na akadiriki kuendelea na msimamo huo hadi alipoachishwa uwaziri wa viwanda na biashara.

Katika utetezi wake, Chami alidai kushindwa kumwondoa mkurugenzi huyo madarakani kwa kile alichodai kuwa mtendaji huyo ni mteule wa Rais kama alivyo yeye. Kauli hiyo, na kubaki madarakani kwa Ekerege, kuliwashangaza wengi ambao waliamini kuwa hakukuwa na sababu ya kutomwondoa kwa vile lengo lilikuwa kutaka tume ya uchunguzi ifanye kazi yake ikiwa huru.

Aidha inajulikana wazi kuwa kusimamishwa sio kufukuzwa, na hivyo angeweza kurudi kazini ikiwa ataonekana hana hatia.

Hata hivyo Dk. Kigoda ambaye ni Mbunge wa Handeni hakuwa tayari kuwataja wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliopewa kumchunguza Ekerege.

Katika hatua nyingine waziri huyo alisema atainua sera ya kukuza viwanda na biashara ikiwemo kuinua wafanyabiashara wadogo na ushirikiano baina ya serikali na viwanda vidogo.

“Tumepanga kuwasaidia wajasiriamali na kuangalia maeneo ambayo watu wakiwezeshwa watainua uchumi wao na kuboresha utendaji kazi,” alisema.
Alisema kiwanda cha General Tyre kitahitaji kufufuliwa na viwanda vya Pamba na Korosho.

Pia alivisifu viwanda vinavyoiingizia serikali mapato kuwa ni kiwanda cha Saruji Twiga, Sigara (TCC) na viwanda vya bia kutaka viwanda vingine kuiga mfano ikiwemo kuongeza juhudi.

Akizungumzia uwekezaji katika nchi, waziri huyo alisema kuwa suala la kupunguza gharama za umeme halijapata ufumbuzi hivyo juhudi zinahitajika kukabiliana na changamoto hiyo.

Chanzo: Tanzania Daima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2012

    mmh!.. Kazi imeanza sasa.
    Na hizi kampuni zake za inspection ya ukaguzi wa Magari nazo zitapigwa Stop hapa UK??

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2012

    Jipumzikie tu baba shida iko wapi make umesimamishwa lakini ka account kanasomeka vizuri hadi mwisho wa mwezi hadi waunde kamati ya kukuchunguza miaka minne, then mashtaka miaka saba na utetezi ukosekane then unarudi kazini kama kawaida sasa hivi fanya biashara tu make unajuana na wafanyibiashara kibaooo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2012

    Safi sana waziri Kigoda. Tunaomba huo uwe ni mwanzo tu na wengine wote walioshiriki kufanya madudu waondolewe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2012

    Well done Kigoda,je na haw a wanae wanakusanya pesa hapa UK utawafanyaje?i hope wataiona segelea .

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2012

    this is really great news!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2012

    The amount of corruption in the public sector is frightening. The level of corruption had migrated from sporadic to a systematic and now an instutionalised form of corruption. The problem is so bad that sn unscrupulous 'mobocracy' is undermining the country's development potentioal. A few mob dominate the resources of this country at the expense of the majority - what a shame!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2012

    bora Kigoda kadhubutu lakini mwezie eti anasingizia presidential appointment alinibore mchga yule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...