KAKA ISSA NADHANI UNAENDELEA VIZURI NA SHUGHULI ZAKO ZA KAWAIDA NA MUNGU AKUPE AFYA ILI UTUONGOZE ZAIDI WATANZANIA TUZIDI KUFUNGUWANA MACHO!

KAKA NIKO NA MASWALI MENGI KWENYE KICHWA CHANGU AMBAYO NAJIULIZA LAKINI SIPATI MAJIBU,NI KWENYE KUHUSU NCHI YETU NA VIONGOZI WETU WANAOTUONGOZA LAKINI HILI LA TANESCO LINANIUMIZA ZAIDI NA SIJUI KWANINI VIONGOZI WETU WANALIZIBIA MASIKIO!

KAKA LEO NIMEPITA TANESCO YA HAPA MKOANI TANGA NIMEKUTA WATU WENGI WANALIA KUHUSU UMEME USIOKUWA NA LUKU,JINSI WATU WANAVYOBAMBIKIWA BILI!CHAKUTIA HURUMA NIMEKUTA WAZEE WENGI WASIO JIWEZA WANALIA KUTOKANA NA WANAVYO PANGIWA BILI NA WAFANYAKAZI WA TANESCO BILA KUWAONEA HURUMA!

NIMEONGEA NA WATU TOFAUTI WENGI WANASEMA BILI YA NYUMA ALILIPA 20,000 LAKINI HII AMEPATA 100,000 NA NIMEPATA KUONGEA NA DADA MMOJA AMBAYE ALIKWENDA MPAKA KWA MENEJA JUU AKANIAMBIA YEYE MWEZI ULIOPITA ALILIPA 47,000 LAKINI MARA HII AMELETEWA BILI YA 197,000 AMEKWENDA KWA MENEJA AMEMWAMBIA COMPUTER HAISEMI UONGO NA NDIO HIYO BILI ANATAKIWA ALIPE,AKAMWAMBIA LABDA HAO WALIOKUWA WAMEPANGA NDANI WALIKUWA HAWALIPI!

SASA KAKA NIMEJIULIZA KAMA HAO WALIOKUWA WAMEPANGA WALIKUWA HAWALIPI KWANINI HIYO BILI AMELETEWA SASA HIVI KWANINI HAIKUJA MWEZI WANYUMA NA KWANINI HAO WAPANGAJI HAWAKUWAKATIWA UMEME?

JIBU NIKWAMBA WAPANGAJI WALIKUWA WANATOWA RUSHWA MPAKA WALIPOHAMA SASA LINAMKUTA MWENYE NYUMBA AMBAPO SIO HAKI!NIKAONGEA NA BIBI MMOJA AKANIAMBIA MMI BABA YANGU HATA ILE TAA SIWASHI MPAKA WAKATI NINATAKA KUSALI NA ANALIPISHWA 97,000 KAKA MACHOZI YALITOKA MAANA SIJUI YULE BIBI HIYO PESA ATAITOWA WAPI NA TANESCO WAMEMWAMBIA ALIPE ZOTE KWA PAMOJA!!

NDUGU ZANGU WA JAMII NINAWAOMBA TUSHIRIKIANE,TUSHIKANE MIKONO KWA PAMOJA TUISAIDIE JAMII NA TUWAOMBE WANASHERIA WAINGILIE
KATI VITU KAMA HIVI AMBAVYO WAKURUGENZI NA MAMENEJA WAMESHAKULA SASA MNYONGE NDIO ANATAKIWA ALIPE HII SIO HAKI KABISA!!

MDAU WA GLOBU YA JAMII KUTOKA TANGA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2012

    MUNGU ANALIPA HAPAHAPA NAWAOMBA TUE TUNALIPA NA REKODI TUNAWEKA WANANCHI KAMA USHAHIDI TUSIKUBALI KUONEWA WENYE ELIMU WAWAPE WAZEE KAMA HUYO ELIMU YA MSAADA JAMANI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2012

    dah inatia huruma sana jinsi wananchi wanavyoonewa. Yaani maskini hana lake akienda hospitali anaonewa shule anaonewa tanesco anaonewa . sijui hii nchi inaenda wapi . kila siku naona tunapiga hatua tatu mbele mbili nyuma alafu tunashashangilia

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2012

    tanesco wanatia kichefuchefu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2012

    Karibu kwenye jehanamu ya Tannesco, sisi tuko Magomeni, tumenyanyasika mpaka basi, hakuna cha waziri Ngeleja wala Mkulo, tupo sisi tu na Mungu wetu-tulisha wahi kuletewa bili ya Million 20-tuna ki-mgahawa cha chips, eti serikali inawasaidia wajasilia mali !! wacha wanunue mashangingi tu hao na maisha ya dunia hii ni yakupita. Labda sasa waziri Muhongo atafanya mabadiliko-lakini , shirika hili !!! Mungu yupo!! kama TTCL imenyoshwa na Vodacom,basi na hawa dawa yao ipo tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2012

    asilimia ya wafanyakazi wa tanesco ni wezi tokea ngazi za juu mpaka ngazi za chini hiyo ni sehemu ya wao kunufaisha matumbo yao na wake zao na vimada mitaani hakuna lingine

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2012

    Ipo siku itapatikana njia nyingine ya kupata umeme na ili shirika litaanguka kifo cha mende. Ubabe wao ni kwa vile hakuna mpinzani lakini nani alijua kama TTCL itafika hapa ilipo. Mabenki nayo matumbo moto kwa sasa baada ya
    M-pesa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2012

    Umeme ni sehemu inayogusa 100% ya mapato ya nchi na uendeshaji wa maisha ya binadamu. Nawashauri viongozi Wapate washauri wazuri kwene Sector hii ili wananchi wapate unafuu wa maisha. Ninamaumivu pia makali ya kulipa Bill ya umeme.Nalalamika nafanya kazi pata picha mzee asiyejiweza,ni ngumu sana. Maoni yangu watafute Consultant wa kuwapa mbinu ya kuiendesha Tanesco,kuna watu wanalipwa kwa kazi iyo na shirika linainuka. TANESCO wanakosa professionalism kwene shirika. Si shirika rahisi kama wanavyofikiria na kulipeleka kizamani. Consultant atawasaidia kujua nchi zingine zinaendeshaje shirika kama hili. Ni hayo tu ya kwangu machache.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2012

    Wabunge hapa ndio pakuchukulia point kwenye hii blog ilikuwasaidia wananchi!sasa kazi kwenu mmeshaonyeshwa uchafu uko wapi!saidia raia!Meneja Tanesco tanga kaa vizuri!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2012

    INASIKITISHA SANA. NATUMAINI KAMA KUNA WAKUBWA WANASOMA BLOG YAKO MICHUZI WENYE MOYO WA UZALENDO WASHUGHULIKIE HII KITU. YAANI INAKATISHA TAMAA KABISA. TUTAFIKA KWELI JAMANI? AFADHALI TURUDI BASI NYUMA KWENYE VIBATARI, HUKO NAKO MAFUTA YA TAA JUU. AHHHHH NIMEJICHOKEA MIE. MUNGU TUNASIDIE, MUNGU ISAIDIE TANZANIA. MAFISADI MLAANIWE.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2012

    Mafisadi ni wengi,kwahiyo watanzania tuamke na tushikamane tusitake kupelekeshwa kama gari bovu,Sasa tumechoka kuonewa kila sehemu,ikitubidi tufanye kama Algeria!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...