WAREMBO watakaoshiriki shindano la Redd's Miss Dar Intercollege 2012 leo wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo kwenye hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema kwamba warembo hao watatoka Chuo  cha Biashara (CBE), Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, pamoja na Ustawi wa Jamii.

“Leo tunaanza mazoezi yetu pale Lamada ambapo warembo kutoka vyuo vinne wataanza kujinoa…wiki ijayo huenda tukaongeza washiriki wengine ambao watatoa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambao wanafanya shindano lao mwishoni mwa wiki hii,”alisema.

Aliendelea kusema kuwa warembo hao watakuwa chini ya ukufunzi wa mrembo aliyepata kushiriki shindano hilo, Rose John, huku kwa upande wa shoo watanolewa na Bob Rich.

Dina aliwataja wadhamini waliojitokeza mpaka sasa kuwa ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Michuzi Media Group na Dodoma Wine, huku akiomba makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo litakalofanyika mwezi ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...