Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya namtumbo Dkt Simon Chacha na Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya hiyo Mussa Zungiza kulia,wakiwaongoza wageni na watumishi wa idara ya afya kwenda kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali katika hositali ya wilaya hiyo, wakati wa sherehe ya siku ya wauguzi Duniani.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Simon Chacha akizungumza na wauguzi wa hospitali hiuyo wakati wa sherehe ya siku ya wauguzi duniani ambayo kiwilaya ilifanyika mjini Namtumbo,kulia mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya hiyo Mussa Zungiza.
Afisa Utumishi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambaye jina lake halikufahamika mara moja akizungumza wakati wa sherehe za siku ya wauguzi wa wilaya ya Namtumbo.kulia ni mganga mkuu wa wila Dkt Simon Chacha na kushoto afisa elimu ya msingi Rhoda Mbilinyi
Askari polisi wa kituo cha Namtumbo mkoani Ruvuma,wakiongoza zoezi la uwashaji mishumaa kama ishara ya upendo na matumaini kwa wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali, wakati wa sherehe za siku ya wauguzi Duniani ambayo kiwilaya ilifanyika katika viwanja vya hospitali mjini Namtumbo.
mhhh maafande wa dot.com
ReplyDeleteAnkal, hivi siku hizi maafane hawanyoi "denge"?(kwa kizazi cha dotcom, denge ni mtindo wa kunyoa wa wakati wa mwalimu hasa kwa maafande.)
ReplyDeleteMaafande Wasichana wamependeza sana!
ReplyDeleteIla wafuate Kanuni, Maadili na Sheria huku wakizingagtia Haki za Binaadamu na sio kuleta 'Muziki wa Kizazi kipya' kazini!
Chachaaaa umetishaaaa by Kaboka
ReplyDelete