Na Woinde Shizza,Arusha
MBUNGE wa jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nasari (chadema) amewasihi vijana,kujifunza uwajibikaji na kuachana na starehe zisizo za msingi hususani unywaji wa pombe wa kupindukia aina ya viroba,hatua ambayo itawasaidia kuwa na maono yenye tija katika kujiletea maendeleo wenyewe na kuondoa dhana tegemezi.
Nasari ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha watoto yatima cha African Orphanage kilichopo Sakila,uzinduzi huo ulienda sanjari na sherehe za kumuaga mwinjilishaji na mwasisi wa makanisa ya Pentekoste wilayani Arumeru,Askofu Nickson Issangya anayeenda kuhubili injili nje ya nchi katika nchi za Afrika na balani Ulaya.
Aidha alisisitiza kwa kuwataka wananchi katika jimbo hilo kushikamana kwa pamoja na kusahau itikadi zao za kisiasa kwani muda wa kampeni umeisha na mbunge amepatikana.
Alisema wakazi wa jimbo hilo wengi wao wamekuwa wakijengeana chuki zinazosababishwa na tofauti za kisiasa hadi makanisani bila kutambua kuwa uchaguzi sasa umeisha na kinachotakiwa ni kuwajibika kwa kufanyakazi za kuleta maendeleo katika jimbo hilo na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine mbunge huyo alitoa ushuhuda wa maisha yake na kudai kuwa wakati akisoma shule ya msingi alikuwa akiuza kwa kutembeza minadani mifuko aina ya plasitiki maarufu kwa jina la Marliboro, kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada.
Alisema kuwa wakati akisoma alipandikizwa maono ya ubunge na mwenyezi mungu ,hivyo katika kipindi chote cha masomo yake kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu,ndoto zilizokuwa zikimjia usingizini ni kuhusiana yeye kuwa mbunge .
Aliwataka wananchi katika jimbo hilo kushikana katika kuliletea maendeleo jimbo la Arumeru mashariki,lenye changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa Ardhi,na kudai kuwa atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha analeta mabadiliko na kwamba wakazi wa jimbo hilo hawatajuta kumchagua .
Kwa upande wa Askofu Nickson Issangya aliwaomba wakazi wa jimbo hilo kuacha kubaguana kwa itikadi za kisiasa hadi makanisani na kuwataka kupigania maendeleo yao wenyewe wakimtumaini mwenyezi mungu kwa kuwa kampeni za uchaguzi zimeisha na mbunge amepatikana.
Katika sherehe hiyo mbunge Nasari aliahidi kusaidia vituo vya watoto yatima vilivyomo katika jimbo hilo na kuwataka wananchi kujikita zaidi kutoa msaada kwenye makundi yasiyojiweza hususani watoto yatima wajane na akinamama wazee,kwani kabla ya kuwa mbunge aliwahi kufanyakazi kwenye kituo cha watoto yatima wapatao 86 .
Na kweli maana kauli alizozitoa nadhani ye mwenyewe alikuwa amepiga VIROBA vya kutosha
ReplyDeletehehehe, kumbe Membe hayuko peke yake!!
ReplyDeleteSafi sana!
ReplyDeleteMhe. Joshua Nassari hayo sasa ndio majukumu ya Ubunge na sio uchochezi vurugu na uvunjaji wa sheria.
Hayo ya 'itikadi hiyo' na 'uenezi huo, utakuwa umeyapata kutoka kwa Wanasiasa waliopevuka na kukomaa kutoka CCM (sio CHADEMA) hapo Arumeru Mashariki!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Hi ni kweli vijana achekunywa pombe kabisaa hakuna faiida yeyote.zaiidi ya ku haribu afya yako tuu mimi mwenyewe nimeaacha kabisa!!! sasa ni mazoezi tuu Asnte mheshimiwa kwa kulioona hilo wanafiri ni fashion furani kunywa pombe laa hasha!! mdau
ReplyDeletemaziku kutoka Amsterdam
Mie NASHANGAA WATU WANAKATAZA POMBE ZA KIENYEJI POMBE NI POMBE TU ZOTE HAZIFAI WACHENI KUONGELEA KITU NUSU NUSU POMBE ZOTE NI MAGONJWA NA DRUG PIA ZINAUMIZA SANA VIJANA TUENDELEE HIVYOHIVYO KUKEMEA HONGERA NASSARI. PAZI.
ReplyDeleteKwa yale aliyosema kwenye ule mkutano wa Chadema ingefaa yeye mwenyewe aache pombe kwanza.
ReplyDeletena yeye aache bangi inayomtuma kutugawa watanzania
ReplyDeletewatakutimua wachaga sasa hivi , hujui kama ni mila yao kunywa pombe na ukisema hivyo masale yatapandwa na nini
ReplyDeletemh. rais wa kanda ya kaskazini angalia !
Huyu jamaa taahira nini, tuache pombe na viwanda vya pombe ndivyo vinavyoilipa serikali. Baba alikunywa mvinyo sisituache kwa nini
ReplyDelete