Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge mteule wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh Shyrose Bhanji wakati wa hafla ya Hepi Besdei ya kuzaliwa kwake iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wa CHADEMA ni Mh.Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum wa chana hicho, Mh. Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Mh Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose Mwwnyewe yenye rangi 'nyutro' kuliwa.
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge wa vyama mbalimbali, wanasiasa, Wasanii wa muziki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.
Ukiondoa kisa hicho cha Keki, hafla hiyo fupi iliyofana sana, ilionesha jinsi waheshimiwa wabunge wetu walivyo na mshikamano katika jamii, na kudhihirisha ukomavu wa kisiasa kwa kushiriki katika shughuli ya mwenzao bila kujali itikadi zao kisiasa. Na cha kusisimua zaidi ni pale ilipowekwa wazi kwamba mameneja wa kampeni wa Mh Shyrose walikuwa Mh Esther Bulaya (CCM viti maalumu) akisaidiana na Dkt Hamisi Kigwangwala kwa upande wa chama tawala, na Mh Halima Mdee aliyekampenia katika kambi ya upinzani akisaidia na Mh Lucy Kiwelu. Picha na Father Kidevu a.k.a Mroki Mroki
Hawa wabunge wa CCM na CDM wamekuwa kama watania wa jadi Simba na Yanga.Tatizo liko kwa wanachama au mashabiki kugombana pasipokuwa na sababu maalumu.Happy Birthday Shyrose (how old are you now?-ni siri yako)na HONGERA SANA kwa kuchaguliwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kusema kweli umepigana kutafuta ubunge mpaka umefanikiwa.
ReplyDeleteSwali la kizushi.Namwona designer wetu Hassanali katika hafla hiyo alituahidi kutupa siri ya kupungua kwake unene lakini naona mpaka leo kakaa kimya.Hongera tena Hassanali kwa kupungua unene.
Hassanali amepungua kwa operation ya kufunga utumbo kidogo inayokufanya ule chakula kidogo ni operation yenye soko kubwa saana sasa India na South Africa utaona kuna watanzania wengi wamefanya operation hiyo haswa wenye asili ya kiasia na kiarabu.
ReplyDeleteHongera Tanzania na waTanzania na wabunge wetu vyama vyote kwa mshikam ano wa dhati na waupendo.
ReplyDeleteHata wa ulaya hawatufikii kwa hilo.Huu ndo utamau wa Tanzania bwana.Ushindani ni katika kuomba kura uchaguzi ukiisha wote ni kaka na dada,baba na mwana.Si mumeona hapo katika birthday!
Kuna watu wachache wahalijui hilo wanatafuta umaarufu kwa kugombanisha ndugu zetu.
Hahahaha,
ReplyDeleteNiacheni nichekeleeeee!
Waheshimiwa wa CHADEMA, msiogope ile ni rangi ya Keki tu (Kijani na njano/ kwa CCM na YANGA) hata kama mkila haitawageuza msimamo wenu wa Kiitikadi wala kuwapa Uhamisho kutokea Msimbazi hadi Jangwani hata kwa Dirisha Dogo wala kwa Usajili Mkuu!!!,
Na huo ndio Mshikamano wenyewe bila kujali Itikadi zetu.
DAIMA TUKO PAMOJA !!!!