Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Ivory Coast, Mh. Allasane Ouattara wakati akimpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jijini Arusha leo. Rais Ouattara ni mmoja wa wageni mashuhuri wataohudhuria mkutano wa afDB jijini Arusha ambao utafunguliwa rasmi na Rais Kikwete.
Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2012

    Jamani DEGE lote hili linamleta mtu mmoja tu? Maskini Afrika Bara Langu!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2012

    mhmmmm umeona enheee kaka maana hata mie ndio naangalia hapa sitaki kuamini kama ni yeyetu ndo kaletwa na hii ndege duh hpn kwa kwelii kwa mtaji huu hatuwezi endelea kamweeeee

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2012

    yep, halafu jumamosi mpira ni wetu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2012

    Kwa hiyo?
    Tatizo Waswahili hamuulizi kwanza kabla hamjahukumu. Sasa angekujaje? Isitoshe, kwa taarifa yako, ndege hizi hulipiwa kila ukiitumia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2012

    Sio mtu mmoja mdau #1, ni delegation. Ni ofisi, sio person, na kila member wa delegation ana kazi yake. Sina nia ya kutetea kuwa na ndege ya hivyo, lakini si sawa kusema ndege emeleta mtu mmoja!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2012

    Mdau hapo juu unasema ulipiwa je analipa nani!?. Si wananchi wanalipia kupitia kodi?? Hilo ndo tatizo langu. Najua ni delegation lakini DEGE hilo lina uweza wa kubeba zaidi ya wato 150 kwani nini hiyo delegation isikodi ndege NDOGO?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2012

    anabeba bureaucracy nzima, anaogopa kupinduliwa!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2012

    hela za mfarasa bwana ndege ya watu karibu mia na inamleta mtu mmoja kwa nini asije na ndege ya abiria wengine ,mwafrika ni mwafrika ndio anataka kubadili ivory coast

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2012

    Jamani jamani, mkuu wa nchi anastahili heshima yake...sasa mlitaka aje na usafiri gani? Mimi nafikiri kifaa cha usafiri cha angani tena kinachombeba mkuu wa nchi kinahitaji kuwa imara kweli kweli...ndege ikiwa ndogo huwa inasumbuliwa na mawimbi na mara nyingi delegation huwa inaondoka na mkuu wa nchi...kwa hapa mimi sioni kosa kabisa....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...