Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Ivory Coast, Mh. Allasane Ouattara wakati akimpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jijini Arusha leo. Rais Ouattara ni mmoja wa wageni mashuhuri wataohudhuria mkutano wa afDB jijini Arusha ambao utafunguliwa rasmi na Rais Kikwete.
Picha na IKULU
Picha na IKULU




Jamani DEGE lote hili linamleta mtu mmoja tu? Maskini Afrika Bara Langu!!
ReplyDeletemhmmmm umeona enheee kaka maana hata mie ndio naangalia hapa sitaki kuamini kama ni yeyetu ndo kaletwa na hii ndege duh hpn kwa kwelii kwa mtaji huu hatuwezi endelea kamweeeee
ReplyDeleteyep, halafu jumamosi mpira ni wetu!
ReplyDeleteKwa hiyo?
ReplyDeleteTatizo Waswahili hamuulizi kwanza kabla hamjahukumu. Sasa angekujaje? Isitoshe, kwa taarifa yako, ndege hizi hulipiwa kila ukiitumia.
Sio mtu mmoja mdau #1, ni delegation. Ni ofisi, sio person, na kila member wa delegation ana kazi yake. Sina nia ya kutetea kuwa na ndege ya hivyo, lakini si sawa kusema ndege emeleta mtu mmoja!
ReplyDeleteMdau hapo juu unasema ulipiwa je analipa nani!?. Si wananchi wanalipia kupitia kodi?? Hilo ndo tatizo langu. Najua ni delegation lakini DEGE hilo lina uweza wa kubeba zaidi ya wato 150 kwani nini hiyo delegation isikodi ndege NDOGO?
ReplyDeleteanabeba bureaucracy nzima, anaogopa kupinduliwa!!!
ReplyDeletehela za mfarasa bwana ndege ya watu karibu mia na inamleta mtu mmoja kwa nini asije na ndege ya abiria wengine ,mwafrika ni mwafrika ndio anataka kubadili ivory coast
ReplyDeleteJamani jamani, mkuu wa nchi anastahili heshima yake...sasa mlitaka aje na usafiri gani? Mimi nafikiri kifaa cha usafiri cha angani tena kinachombeba mkuu wa nchi kinahitaji kuwa imara kweli kweli...ndege ikiwa ndogo huwa inasumbuliwa na mawimbi na mara nyingi delegation huwa inaondoka na mkuu wa nchi...kwa hapa mimi sioni kosa kabisa....
ReplyDelete