Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni juu ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba(kulia) akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipomtembelea ofisi kwake jana.Wengine katika picha ni Makamu mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu Mstaafu Mhe. Agostino Ramadhani(Watatu kushoto),Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Mathias Chikawe(Wapili kushoto) na kushoto ni naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angela Kairuki.
Rais akizungumza na wajumbe wa tume hiyo katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la tume hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Profesa Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe wa Tume ya kuratibu maoni kuhusu katiba wakati Rais alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba wakati alipotembelea ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
Inatia moyo sana kuwa na watu makini kama hawa. Ninaamini kabisa kuwa timu itapenda kuwa katika legacy kwa miaka 100 ijayo. Ila haitakuwa rahisi kwa kuipata legacy hiyo kama hawatakuwa tayari ku-resist pressure toka kwa wanasiasa. Wanasiasa wao wanaangalia vyama vyao na ustawi hivyo.
ReplyDeleteHawa wajumbe wa tume tume wanatakiwa kuangalia zaidi Tanzania isiyokuwa na chama chochote cha siasa zaidi ya watanzania walioungana wenye demokrasia ya kweli na wenye uwezo wa kuchagua mtu yeyote kutoka chama chochote au hata kama hana chama kuwa kiongozi wao.
Nina hakika kabisa kuwa tume ikizingatia haya basi tutapata katiba si tu ya kutupeleka miaka 50 ijayo bali hata 100 au 150 ijayo. Anything short of that watakumbukwa tu kama waliwahi kuwa wanatume ila hawatakumbukwa kwa product ya tume yao maana haitakuwepo, we will all fail of future generation.
Lakini pia mafanikio ya tume hii kuja na katiba isiyo na pre-conceived interest za kulinda nani na kuangamiza nani kutamfanya JK akumbukwe na vizazi na vizazi vijavyo. Otherwise tume hii na rais huyu watasahaulika kama tume nyingine zilizowahi kuwekwa na marais waliopita huko nyuma
Nina Imani na Warioba, nina imani na Dr Salim, Nina Imani Baregu na kwa maana hiyo basi inanifanya niwe na imani na wanatume karibu wote.
Hivi sababu hasa ya hawa viongozi kwenda kuitembelea hii tume ni nini?Naomba kuelimishwa.
ReplyDeleteKama na professor Baregu yupo kwenye mchakato huu basi sina wasiwasi, chakula kitatoka jikoni kimeiva vizuri, I know this guy.
ReplyDelete