'Wilaya ya Handeni inabahati ya kupata wakuu wa wilaya warefu, tazama mimi mrefu na anayenipokea naye mrefu kama mimi', ndivyo alivyokuwa akisemaaliyekuwa mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya ya Handeni Kapteni Mstaafu, Seif Mpembenwe (katikati) akimweleza Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe, Bw Sadick Kallaghe, kulia ni Bw. Muhingo Rweyemamu mkuu mpya wa wilaya ya Handeni.
Picha na Habari na Mashaka Mhando,Tanga
Mkuu mpya wa wilaya ya Tanga, Bi Halima Dendegu akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa katika sherehe ya kuwaapisha wakuu wa wilaya katika wilaya nane za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa wilaya mpya ya Korogwe, Bw. Mrisho Gambo ambaye alikuwa mmoja ya wagombea ubunge wa Afrika Mashariki, akila kiapo chake mbele ya Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa.
Aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mtanzania, Bw. Muhingo Rweyemamu, akitia saini hati zake za kiapo mara baada ya kuapa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu, Chiku Gallawa.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa (mwenye kilemba chekundu katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya hao mara baada ya kuapa, kutoka kushoto ni Bi Hafsa Mtasiwa (Pangani), Bw. Selemani Liwowa (Kilindi), Bi Halima Dendego (Tanga), Bw. Muhingo Rweyemamu (Handeni), Bw. Majid Hemed Mwanga (Lushoto), Bw. Mrisho Gambo (Korogwe), Bi Mboni Mgaza (Mkinga) na Bi Subira Mgalu ambaye ni mkuu mpya wa wilaya ya Muheza 'Bonde'.
Picha na Habari na
Mashaka Mhando,Tanga
MUDA mfupi tu baada ya kuapishwa na kukabidhiwa vitendea kazi katika wilaya ya Korogwe,Mkuu mpya wa wilaya hiyo Mrisho Gambo anaahidi kuanza mara moja kupitia kurasa kwa kurasa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali(CAG)kuhusiana na mapato na matumizi ya wilaya hiyo.
Akizungumza katika mahojiano na Gazeti hili jana Gambo alisema kuwa miongoni mwa mikakati yake ni kuangalia mipango ya maendeleo ya miaka mitano ya wilaya hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa inatekelezeka.
“Cha kwanza kabisa ni kupitia ripoti ya CAG kwa upande wa Korogwe na hii nitaipitia kurasa moja moja na mkakati mwingine ni kuangalia mipango ya maendeleo ya miaka mitano na utekelezaji wake ili nione wapi tunapaswa kuelekea”,alisisitiza Gambo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa aliaahidi kuhakikisha kuwa ataintangaza wilaya hiyo katika Nyanja za kiutalii kwa ngazi ya Taifa na kimataifa ikiwa ni hatua moja wapo ya kuongeza fedha za kigeni ndani ya nchi na hatimaye kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
“Ninachowaomba wananchi na Viongozi wa Pangani ni Ushirikiano wao hasa katika hili suala la utalii ninachotaka Pangani itambulike kimataifa na iwe Pangani ya sasa kwa maana ya maendeleo”,alisema Mtasiwa.
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Galawa aliwataka Wakuu hao wa wilaya nane za mkoa wa huo kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasiha wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi kwa lengo la kupata mnyoro wa mafanikio.
Galawa alisema ushindi unapatikana hasa pale ambapo viongozi hao watafanikiwa kutatua changamoto,kero na migogoro ya wananchi huku wakilenga kuiboresha na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kutokana na rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao.
“Bahati ya pekee kuwa mkoa wa Tanga una fursa mbalimbali za kiuchumi lakini kwa nini hazitumiki hilo ni suala la sisi wenyewe kama viongozi kulivalia njuga na kuwahimiza wananchi katika kuzichangamkia ….tuwe karibu na wananchi tuwaelimishe,tuwahamasishe ili kwa pamoja tusonge mbele hatuhitaji kusinzia”,alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Wakuu wa wilaya walioapishwa ni Pamoja na Muhingo Rweyemamu(Handeni),Halima Dendego(Tanga)Hafsa Mtasiwa(Pangani),Mboni Mgaza(Mkinga),Subira Mgalu(Muheza),Majid Mwanga(Lushoto),Selemani Liwoa(Kilindi),Mrisho Gamba(Korogwe).
Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi hasa baada ya kufa kwa viwanda.
Hongera sana DC wa Mkinga Bi. Mboni Mgaza
ReplyDelete