Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na mchezaji soka nyota wa Uingereza anayechezea Los angeles Galaxy ya Marekani, David Beckham, walipokutana uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London Jumatano, muda mfupi kabla ya Rais Kikwete na Mama Salma kuelekea Washington DC kuhudhuria mkutano wa G8 kwa mwaliko wa Rais Barak Obama wa Marekani. Bekham ameonesha nia ya kutembelea Tanzania kama mtalii siku za karibuni na Rais Kikwete amemkaribisha kwa mikono miwili, akimhakikishia kwamba licha ya kuwa na mashabiki wengi ambao watafurahi kumuona pia atafurahia vivutio kibao vya kitalii.
Picha na mdau Amos Msanjila
Tunamkaribisha beckham hasa sisi washabiki wa man u.
ReplyDeleteMhe. Raisi JK mkaribishe Tajiri Beckham aje atuchangie na sisi kwa Utalii atakao fanya kwetu!
ReplyDeleteI wish ningekutana na Beckham nimpe maelezo ya kina juu ya uzuri na vivutio vya nchi yetu Tanzania is the best of Africa.
ReplyDeleteKipepeo Tours
SAFI SANA JK UKIPATA NAFASI NA ICON KAMA HAO UNAITUMIA FULLY
ReplyDeleteKARIBU BECKHAM
JK: Hi David, I am JK, and this is my wife Salma, I am president of Tanzania.
ReplyDeleteDB: Hello, JK, nice to see u, Tasmania, is that an island off Australia?
JK: No, in Africa.
DB: Oh! sorry, is that near Kruger national park?
JK: No, east coast.
Aje awekeze katika soka la vijana aanzishe shule angalau 1 ya soka la vijana
ReplyDelete