Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania kupitia kampuni ya Lino Ntenational Agency, Hashim Lundenga akizungumza na baadhi ya washiriki wa shindano la Redds Miss Kurasini jioni ya leo Mei 22,2012 wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika Ukumbi wa Equator Grill jijini Dar es Salaam. Redds Miss Kurasini imedhaminiwa na NAEEMS WAER , wauzaji wakubwa wa nguo za aina zote jijini Dar es Salaam wenye maduka yao Kariakoo na Mwenge, linataraji kufanyika Mei 25, mwaka huu ukumbini hapo. 
 Lundenga aliwataka warembo hao kujiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.
 Kamati hiyo pia ilihudhuria na Katibu Mkuu wake Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye, Ofisa Habari, Aidan Ricco na Ofisa wake Yason Mashaka.
 Warembo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mashindano hayo kitaifa, Hashim Lundenga. 
Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Kurasini wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kuzungumza na Kamati ya Miss Tanzania. 

Wakati Nameems Wear wakiwa ni wadhamini wakuu, wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.

Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20),Linda Deus (20),Irene Sostheness 20),Neemadoree Sylvery(29),Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22)      na Sia Kimambo (19).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2012

    Hii picha inazungumza mengi: kamati ya Miss Tanzania yote ni wakaka na washindani wote ni wadada. Is there something am missing?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2012

    Hivi Lazima hawa wamiss wawe wembamba? Miye skubaliani na hili!

    Hata kama mtu si kuwa mnenenee wa obesity, jamani maumbile ya waTZ wanamama si haya haaaaa hawa wamekondeanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. Mwangwita ChrisMay 23, 2012

    hapo lundenga unafurahi kuona vipaja vya hao wanyange kazi kweli kweli,hiki ni kipindi cha kamati ya lundenga kupata mishiko ya nguvu yetu machooooooooooooo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2012

    Hebu angalia hiyo meza jinsi ilvyochoka!! Yaani.........!!! Na watu ndio hapo hapo wanafanya mkutano, ujanjaujanja tu!

    ReplyDelete
  5. MkomunistiMay 23, 2012

    Huyu Boss wa Miss Tz. amepitwa na wakati na umri umemtupa mkono aachie vijana wabunifu labda wanaweza kutufikisha mbali kimataifa! kila siku lundenga na hamna kitu.

    Wadhamini jitoeni kwani hakuna jipya wekezi ktk mambo ya maana na yenye maslahi kwa wengi kuliko huu upuuzi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2012

    Hivi ili kuwa mrembo lazima uache mapaja nje, jamani watanzania tuache ulimbukeni, sasa si mvue kabisa? Unaweza kuvaa nguo ya heshima bila kuacha mapaja na matiti nje na urembo wako ukaonekana

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2012

    Urembo ni pamoja na mzingira mazuri Mh Lundega, hiyo meza hapo haistahili kutumiwa hata na Mama lishe wa gomapembe let alone miss whatever kambi lol.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2012

    Very interesting...!! Waandaji ote kina kaka af washindani kina dada....duuuh!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2012

    Yah that Commitee isnot gender sensitive

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2012

    Hakuna hat dada mmoja alyelalamika

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2012

    Mdau wa kwanza umesema neno. Hivi hakuna wamama wa kuendesha hay mashindani ya mabinti?

    Hiyo meza aliyoandaliwa Lundenga nemeipenda!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2012

    Hiyo meza ilivyochakaa. Sijui walikosa meza safi na nzuri. Kweli bongo tambarare.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2012

    Hivi wewe Lundenga kwa mavazi na mikao waliyokaa washiriki wa miss Kurasini mwanao anaweza kushiriki?
    hivi haya mashindano ni mpaka wavae na kukaa mikao ya hasara namna hiyo?
    lundenga wewe una watoto wakike kweli,mtu mzima kabisa unawadhalilisha watoto wa wenzio kisa hela? moto unakusubiri wewe usiye na heshima wala adabu!
    mvalishe na mkalishe binti yako hivyo mbele ya kadamnasi!
    SHAME UPON YOU LUNDENGA!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2012

    Tell me a out it

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2012

    Wanawake sio matapeli

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2012

    na hiyo meza du!!! jamani tujitahidi hata kuweka kanga juu meza nayo safi du.

    Ni hayo tu ni mimi

    Mr Nyamaimewahi Kunikabashingoni

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2012

    Hawa viongozi wa u-miss hakuna kustaafu kweli!Toka mambo haya yameanzishwa upya Lundenga Lundenga Lundenga tu.Hii ndo nini jamani.


    Nasehemu zingine hivi hivi watu huzeeka na nyadhifa.Hivi ndo utaratibu gani huu.

    Tulitoka enzi za kina Kubaga,Masauni,Bayi,sasa Tenga Tenga Tenga.Hapa kweli turakuwa tunapata mabadiliko katika mambo yetu!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 23, 2012

    Mnhhh !!!

    Hiyo meza aliyokaribishwa Bwana Mkubwa Lundenga ni kama vile meza ya kukatia supu au kuwekea mabakuli ya supu ya utumbo!

    Ahhh Lundenga ni Mkubwa wenu inabidi mumpe nafasi yake ,kulikoni? vipi Waandaaji Miss Kurasini ???

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2012

    ATI NI KWELI NI LAZIMA AONJE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...