Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.

Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.

Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2012

    Ningeshauri tutumie wachezaji wa under 23 ili baada ya miaka miwili hivi wawe wameiva. Tunaweza kuongeza wakubwa kama watatu tu wa kuleta changamoto na uzoefu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2012

    Du, naona wachezaji wa yanga wanaendelea kula jeuri ya kumpiga refa. Kikosi kizima ameteuliwa mmoja tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2012

    Hamna kitu..Hawa karibu 90% walishashindwa..jaribuni 'fresh legs'.Kuna mdau mmoja kwenye hii blog ya jamii alichangia sikumbuki ni mawaziri wa juzi au..anyway,aliongelea kutoa chungwa kwenye kikapu na kuweka ndimu.

    David V

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2012

    Yanga mmoja tu, sawa tutakutana taifa

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2012

    Hii si timu ya kuifunga Ivory Coast.

    ReplyDelete
  6. Mmmmh hii kali yaani kufugwa 5 ndo imekuwa hatujui mpira nini? je uamuzi wa kocha mkuu ndo wa mwisho? YANGA OYEEEEE!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2012

    Hii ni Simba SC. au Taifa Stars, huyu kocha atakuwa katumwa!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2012

    Amini Amini nawaambia, huyu kaanza vibaya na sababu mnaijua. Kama hamtaniamini subirini hatima yake.
    Pole Kim, busara ndogo imekuponza.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2012

    Huyo ni kocha wa timu ya Taifa au ni Kocha wa timu ya Simba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...