LEONARD G. KANZA NA CHRISTINE T. KANZA
Wapendwa wetu, ilikuwa siku, wiki, mwezi na hatimaye leo tarehe 01/05/2012 mmetimiza miaka mitatu (3) toka mtutoke kwa ajali ya gari katika hii dunia. Tunafarijika kwa sababu tuna Imani mpo pamoja nasi Kiroho siku zote.
Hakuna siku ipitayo kwetu bila kuwakumbuka kwa UPENDO, UKARIMU, USHAURI MWEMA, MSIMAMO BORA NA BUSARA ZENU. Hakika BUSARA ZENU zimekuwa dira na nuru katika maisha yetu. Tunaendelea kuwaombea na tutaendeleza yale yote mema mliyotuachia.
Daima mnakumbukwa na watoto wenu, Bright Kanza na Alvin Kanza, Mr & Mrs T. Kweka, Mr & Mrs G. Kanza, wadogo zenu wote, wajomba, shangazi, ndugu, jamaa na marafiki. Daima tutawakumbuka Milele.
Sisi tuliwapenda sana, lakini Mungu Baba wa Mbinguni aliwapenda nyinyi zaidi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. Amen!!
Ni ngumu kuamini kwamba hamko hai Christina na Leonard, ni maobi yangu watoto wenu Bright na Alvin wakuzwe katika kumjua Kristo kama mlivyokuwa Bright an Alvin Mungu yuko nanyi haawaacha. Wazi wote Mungu anaendelea kuwatia nguvu.
ReplyDeleteAse, USA
Mimi siwafahamu lakini natoa pole sana kwa wote mlioguswa na msiba huu wa ghafla.Picha imenisikitisha sana baada ya kuona mmoja wa watoto wao nadhani(aliyezibwa na Maua).
ReplyDeletePumzikeni kwa amani.Amen
David V
Wow, huyu jamaa alikuwa school mate wangu o level na A level na tulimaliza udsm pamoja, pia tulikuwa tunakutana sana mitaa ya Ar na Dsm ila sikumwona mida nikajua mizunguko kumbe ndio hivyo tena. Rip wapendwa na pole kwa familia
ReplyDeleteJamani ajali ilitokea wapi? Inasikitisha sana .Mungu awabariki watoto wao.
ReplyDeleteMay God the Almighty father continue to rest your souls in eternal peace. Ninyi mmetangulia, nasi tuko nyuma. Mungu awabariki watoto wenu nao waishi wakijua kuwa bwana ndie atoaye na achukuaye kondoo wake. God bless all.
ReplyDeleteaisee! inasikitisha sana
ReplyDeleteSo sad. RIP Dears.
ReplyDeleteMpunzike kwa amani. Mungu awe pamoja na watoto wenu.
ReplyDeleteMungu aweke roho zenu mahali pema peponi kwa hakika kila nafsi itaonja mauti.
ReplyDeleteMungu awaangazie mwanga wa Amani na awapumzishe kwa Amani mbinguni Leonard na Christine.Awakinge, awaongoze na awalinde malaika wenu Bright na Alvin!
ReplyDeletehata mie siwafhamu ndugu hawa.Lakini Bwana atoaye na ndye atwaaye aziweke roho zao mahali pema peponi.Awakuze watoto wao Alvin na Bright wamjue na kumcha Mungu siku zote za maisha yao.
ReplyDeleteMdau
South Korea
JAMANI NAMI NAUNGANA NA WAPENDWA WENGINE KUWAPA POLE HAWA WATOTO WALIOACHWA NA HAWA MAREHEMU
ReplyDeleteILA WAPENDWA NAOMBA MFAHAMU NENO MOJA KWAMBA WAFU HAWAOMBEWI LOLOTE NA WAKAFAHAMU AU MUNGU KUBADILISHA NENO LOLOTE JUU YAO
BIBLIA INASEMA KWAMABA MTU AKIFA ANRUDI MAVUMBINI NA ATAKAA HAPO MPAKA SIKU YESU ATAKAPORUDI NDIPO KWA NGUVU ZAKE ATAWAFUFUA WALE WALIOKAA KWA IMANI
NA HISTORY YAO IMEFUNGWA SIKU WALIPOKUFA KWAHIYO HATA KAMA TUOMBE MUNGU HAPOKEI TENA OMBI LOLOTE DHIDI YAO WAPENDWA WETU
WAFU PIA HAKUNA MAHALI AMBAPO WATALAZWA PEMA AU PABAYA HUKO WALIPO
ASANTENI WAPENDWA
Dddah! siwajui lakini NIMEUMIA SANA! poleni sana wafiwa !
ReplyDeleteMungu awalaze mahali pema peponi. Bright and Alvin, ur parents are watching over u, mkae salama.
ReplyDelete