LEONARD G. KANZA NA CHRISTINE T. KANZA

Wapendwa wetu, ilikuwa siku, wiki, mwezi na hatimaye leo tarehe 01/05/2012 mmetimiza miaka mitatu (3) toka mtutoke kwa ajali ya gari katika hii dunia. Tunafarijika kwa sababu tuna Imani mpo pamoja nasi Kiroho siku zote.

Hakuna siku ipitayo kwetu bila kuwakumbuka kwa UPENDO, UKARIMU, USHAURI MWEMA, MSIMAMO BORA NA BUSARA ZENU. Hakika BUSARA ZENU zimekuwa dira na nuru katika maisha yetu. Tunaendelea kuwaombea na tutaendeleza yale yote mema mliyotuachia.

Daima mnakumbukwa na watoto wenu, Bright Kanza na Alvin Kanza, Mr & Mrs T. Kweka, Mr & Mrs G. Kanza, wadogo zenu wote, wajomba, shangazi, ndugu, jamaa na marafiki. Daima tutawakumbuka Milele.

Sisi tuliwapenda sana, lakini Mungu Baba wa Mbinguni aliwapenda nyinyi zaidi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. Amen!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Ni ngumu kuamini kwamba hamko hai Christina na Leonard, ni maobi yangu watoto wenu Bright na Alvin wakuzwe katika kumjua Kristo kama mlivyokuwa Bright an Alvin Mungu yuko nanyi haawaacha. Wazi wote Mungu anaendelea kuwatia nguvu.

    Ase, USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    Mimi siwafahamu lakini natoa pole sana kwa wote mlioguswa na msiba huu wa ghafla.Picha imenisikitisha sana baada ya kuona mmoja wa watoto wao nadhani(aliyezibwa na Maua).

    Pumzikeni kwa amani.Amen

    David V

    ReplyDelete
  3. Wow, huyu jamaa alikuwa school mate wangu o level na A level na tulimaliza udsm pamoja, pia tulikuwa tunakutana sana mitaa ya Ar na Dsm ila sikumwona mida nikajua mizunguko kumbe ndio hivyo tena. Rip wapendwa na pole kwa familia

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2012

    Jamani ajali ilitokea wapi? Inasikitisha sana .Mungu awabariki watoto wao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2012

    May God the Almighty father continue to rest your souls in eternal peace. Ninyi mmetangulia, nasi tuko nyuma. Mungu awabariki watoto wenu nao waishi wakijua kuwa bwana ndie atoaye na achukuaye kondoo wake. God bless all.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2012

    aisee! inasikitisha sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2012

    So sad. RIP Dears.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2012

    Mpunzike kwa amani. Mungu awe pamoja na watoto wenu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2012

    Mungu aweke roho zenu mahali pema peponi kwa hakika kila nafsi itaonja mauti.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2012

    Mungu awaangazie mwanga wa Amani na awapumzishe kwa Amani mbinguni Leonard na Christine.Awakinge, awaongoze na awalinde malaika wenu Bright na Alvin!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2012

    hata mie siwafhamu ndugu hawa.Lakini Bwana atoaye na ndye atwaaye aziweke roho zao mahali pema peponi.Awakuze watoto wao Alvin na Bright wamjue na kumcha Mungu siku zote za maisha yao.
    Mdau
    South Korea

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2012

    JAMANI NAMI NAUNGANA NA WAPENDWA WENGINE KUWAPA POLE HAWA WATOTO WALIOACHWA NA HAWA MAREHEMU
    ILA WAPENDWA NAOMBA MFAHAMU NENO MOJA KWAMBA WAFU HAWAOMBEWI LOLOTE NA WAKAFAHAMU AU MUNGU KUBADILISHA NENO LOLOTE JUU YAO
    BIBLIA INASEMA KWAMABA MTU AKIFA ANRUDI MAVUMBINI NA ATAKAA HAPO MPAKA SIKU YESU ATAKAPORUDI NDIPO KWA NGUVU ZAKE ATAWAFUFUA WALE WALIOKAA KWA IMANI
    NA HISTORY YAO IMEFUNGWA SIKU WALIPOKUFA KWAHIYO HATA KAMA TUOMBE MUNGU HAPOKEI TENA OMBI LOLOTE DHIDI YAO WAPENDWA WETU
    WAFU PIA HAKUNA MAHALI AMBAPO WATALAZWA PEMA AU PABAYA HUKO WALIPO
    ASANTENI WAPENDWA

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 02, 2012

    Dddah! siwajui lakini NIMEUMIA SANA! poleni sana wafiwa !

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 02, 2012

    Mungu awalaze mahali pema peponi. Bright and Alvin, ur parents are watching over u, mkae salama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...