Maandalizi ya Mashindano ya REDD’S MISS TANZANIA 2012 yanaendelea kushika kasi kwa ngazi za vitongoji mbalimbali vya jijini Dar es Salaam , Baada ya kufanyika kwa mashindano katika vituo vya UKONGA, CHUO CHA USTAWI WA JAMII na CHUO CHA FEDHA (IFM) sasa ni zamu ya REDD’S MISS KURASINI 2012.
Katika mashindano ya mwaka huu kituo hiki cha Kurasini kitafanya shindano lake siku ya Ijumaa ya tarehe 25 / 5 / 2012 katika Ukumbi wa EQUATOR GRILL uliopo mtoni saba saba.
Jumla ya Warembo kumi na sita mpaka sasa wamejitokeza katika kuwania taji la REDD’S MISS KURASINI 2012 ambalo linashikiliwa na MWAJABU JUMA ambaye pia ni mshindi wa shindano la TOP MODEL 2011 katika fainali za Miss Tanzania 2011, pia ni miongoni mwa warembo waliofika katika fainali ya mashindano ya urembo ya MISS TANZANIA 2011.
mazoezi ya warembo wa Miss Kurasini 2012 yanaendelea katika ukumbi huo wa Equator Grill chini ya walimu wao Top Model MWAJABU JUMA na ROSE HERBERT kwa upande wa SHOO,
Orodha ya majina ya warembo na umri wao ni kama ifuatavyo:-
1. TULEKENE SETH (20) 2. ANGLE GASPER (19)
3. CHRISTINA MOSES (22) 4. ZUHURA SADIKI (21)
5. FLAVIANA MAEDA (22) 6. MWANAISHA ZUBERI (21)
7.FARIDA MROPE (23) 8. IRENE SOSTHENES (20)
9. EDINA MAGIGE (22) 10. SIA KIMAMBO (19)
11. NZELANI JUMA (22) 12. LILIAN JOSEPH (20)
13. ANNA ZAKARIA (21) 14. ASHA MUSA (21)
15. LINDA DEUS 16.BETTY PETER (22)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...