Mwanamama ambaye hakufahamika jina lake kwa haraka,akiwa na sinia lililosheheni Samaki wa Kukaanga aina ya Perege na Kambale aliokuwa akiwauza kwenye stendi ya mabasi ya Mikoani,Ipogolo Mkoani Iringa mchana wa leo.swala la usalama wa afya ya mtumiaji halijazingatiwa kabisa kwa mama huyu kwani samaki hao hawajahifadhiwa katika hali ya usafi.
Mama huyo akikimbilia kwenye Basi ili aweze kuuza samaki hao kwa abiria waliopo ndani ya Basi hilo.
hujalazimishwa kununuwa usituletee zakuleta hapa, hicho chakula hakina tatizo lolote
ReplyDeletewache wenzako wapate riski zao
Hao ni samaki au kuku?
ReplyDeleteMtumiaji anatakiwa akawapashe moto mwenyewe nyumbani kwake,huyo mama hapo labda anahangaikia watoto wake,bwana mkubwa hatoi hela ya matumizi,n.k....watoto wanafika hadi chuo kikukuu(nina mfano halisi).Sikubaliani na kutozingatia masharti ya Afya lakini Ukweli ndiyo huo.Tuliokulia huko vijijini ndiyo 'usipime'.
ReplyDeleteDavid V.
Nani amekwambia haijali afya?? ....nyie wabeba box mmekimbia nchi mkirudi mnajifanya mnajua ''usafi''....kwa taarifa yako Samaki wanapokaangwa wanawekwa CHUMVI ambayo inazuia microbial spoilage by inhibiting growth of food-borne pathogens such as Salmonella or Clostridium botulinum,so hao samaki ni safe na ni watamu ile mbaya,mbona sisi tunakula na hatuumwi???
ReplyDeleteHaaa tena miye huku Toronto natokwa na mateeee, I grew up eating that, mama (RIP) ananunua vipande kadhaa, anatengeneza mchuzi wa nazi anavidumbukiza haaa na ugali na mchicha pembeni, I am where I am today, sijapata minyoo wala kipindupindu....
ReplyDeleteKUNA STUDY ILIFANYIKA UNIVERSITY OF NAIROBI KUHUSU VYAKULA VYA BARABARI, HAVIKUWA NA SERIOUS EFFECT KWA WALAJI. TUACHE TABIA YA KUJIFANYA WAJUAJI. HAIWEZEKANI WATU WOTE TUKAFANYA KAZI ZA AINA MOJA. TUJIFUNZE TUHESHIMU AJIRA ZA WENGINE. NA WEWE UNAEPONGA TULIOKO NJE, HII HABARI INA UHUSIANO GANI NASI. KAMA ULIPIGWA BOMBA KIMPANGO WAKO ACHA HU HATE
ReplyDeleteUsinunue basi, kwani umelazimishwa??
ReplyDeletekuna watu humu fikra hawana.
ReplyDeleteYaani kanuni za afya hazifuatwi halafi wewe unasema "usinunue" au "umelazimishwa?"
Kumbuka kanuni za afya zinamlinda mtu asiyezifahamu wala kuzijali ikiwemo wewe.
muige mwehu kula jalalani basi.
Huyu jamaa ameniharibia siku yangu kabisa. Hao samaki angeweza kuja nao Dar tungegombania. Wakiwekwa nazi, na punga pembeni. Nomaaaaaa!
ReplyDeleteSio kila unachokiona huko ulaya ni kweli. Hakuna tatizo hata kidogoooo la afya. Pumbafu!
KAZI NI KAZI BORA MKONO UENDE KINYWANI!!
ReplyDeleteHuyu mama nimempenda, ajira hakuna, bora alivyoamua kufanya hivyo kuliko kuwa ombaomba au changuduo. Bravo mama, hali ya maisha imekuwa ngumu sana hata sasa naona hapa Dar biashara ya kuuza matunda (ndizi, karoti, mapapai, parachichi) ni akina mama walio na mabeseni vichwani wanazunguka kila kona na wengine wakiwa na watoto migongoni.
Mama ni nguzo ya familia, usafi umezingatiwa hapo. Mbona twala ndizi mbivu barabarani bila kuosha?
Samaki watamu sana hawa, na ukiwapasha moto basi umeharibu utamu . . . "Mama chachandu ipo hapo?".
ReplyDeleteHujalazimishwa kununua nenda kale vya nyumbani kwako unavyopikiwa na house girl/boy asiyezingatia usafi
ReplyDeleteAliyepost hii habari inabidi ajifunze zaidi, kama ana elimu haimsaidii kabisa. Hii sio njia ya kueleza mazingira ya usafi kwa kumpiga picha mtu hadharani. Alafu hao samaki wamekaushwa ili wawepo muda mrefu, ukinunua unapika au wewe ukinunua unakula bila kuwatayarisha kwanza?. ULIZA KWANZA SIO KUKURUPUKA
ReplyDeleteTusiige mambo ya mamtoni, extreme sanitation and cleanliness is not good for us, the body needs a bit of them bugs to create active its own immunity, no bugs exposure leads to pure immunity and less resitance to diseases.
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.
WEWE BADALA YA KUANDIKA MATAMANISHI UNATULETEA UBWANA AFYA WAKO? HAO NDIO SOMBA BWANA EBO!
ReplyDeleteChakula cha barabarani hakina madhara makubwa kama vya makopo na hayo ma burger na Sausages tunayokula kwa ushahidi tizama watu wanavyo nenepa umarekani na nchi za ulaya ni ugonjwa mtupu na siyo sababu ya kuiba pesa kama TZ.
ReplyDeletewakati mwingine muangalie vitu vya kupost humu hao samaki ni poa sana na mama anapata riziki yake unafikiri atasomesha vipi watoto ?
ReplyDeleteserikali inatoa elimu bure? achenmi kuwa na ujinga mwacheni mama apate riziki
nipo ulaya lakini mate yananitoka nawatamani kishenzi ningekuwa hapo mbona ningemuuingisha mama mpaka akifika nyumbani akanisimulie.