Maharusi,Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali waliofika ndani ya kanisa la Azania Front,mara baada ya kufunga ndoa takatifu,mapema leo mchana jijini Dar.
Maharusi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja mapema leo ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi wakilishana kiapo cha ndoa mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliofika kanisani hapo mapema leo mchana kuishuhudia ndoa hiyo ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi,iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania Front.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya maharusi hao kuvishana.
 Baadhi ya Wanakwaya kutoka mkoani Arusha wakiimba
Umati wa watu uliofika kuishuhudia ndoa ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi iliyofanyika mapema leo mchana ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi wakiingia ndani ya kanisa la Azania Front mapema leo mchana,tayari kwa kufunga ndoa takatifu.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakishuhudia pia tukio hilo adhimu  na la kihistoria kwa Wanandoa.
Maharusi Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiwa na wapambe wao wakielekea kanisani,tayari kwa kufunga ndoa takatifu,mapema leo mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2012

    Hongera sana Bw ba Bibi Metili! Kila la heri katika maisha ya ndoa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2012

    OMG! I am so happy for Ssanyu......wishing u n urs blessings always

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2012

    CONGRATULATION PRINCE WILLIAM AND PRINCESS KATE.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2012

    You look soo beautiful Ssanyu. We wish we were there Sweetie

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2012

    Hongera sana mchungaji mwanafunzi bwana Oltesh Eliguard Metili kwa kupata jiko. Tunaamini ndoa yako itakuwa ni mfano wa kuigwa na watu wote. Kila la heri katika maisha ya unyumba.

    Mdau usharika wa Mbezi beach!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2012

    mmpendeza tatizo la KKKT yetu harusi za viongozi na watu mashuhuri basi askofu ndo anafungisha mmh!! Bibie mbona hajafunika mabega kama msimamzi? upendeleo

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2012

    Siyo kupendeleana bali ni kuzingatia itifaki. Kanisa la KKKT lipo kiitifaki zaidi!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2012

    jamani hongereni sana pia mmependeza sana tu;ila mimi kidogo naomba msaada wa haya majina yenu ni magumu sana na ndio mara ya kwanza kuyasikia hapa bongo,hivi nyinyi ni wabongo?au mumekuja kufanyia harusi hapa bongo tu?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2012

    CONGRATULATIONS DEARS LOOKING GOOD AND HAPPY, THATS WHAT LIFE IS ABOUT, TAKE CARE AND STAY BLESSED

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2012

    Hongera sana Kaka Metili na wifi Ssanyu. Mmependeza sanaaaaaaaaaa. Wewe anon. wa saa Sun May 20, 08:58:00 PM 2012 kwani wabongo manake nini? Acha ushamba, mtu yeyote anaweza kuwa mbongo. Wewe tu ndio hujui majina hayo. Usitake kujidai unajua majina yote ya Kitanzania.
    Nawewe anony. wa Sun May 20, 01:22:00 PM 2012, hapo itifaki imezingatiwa. Metili ni mchungaji mtarajiwa na anatokea usharika wa Azania. Kabla ya hapo alikua mzee wa kanisa wa siku nyingi na Malasusa ndio mchungaji wake na baba yake wa kiroho hata kabla hajawa askofu. Lowasa pia ni family friend wa metili toka zamani hata kabla ya kuwa mbunge. Acha umbea na majungu wewe. uliza kwanza upate uhakika kabla hujaanza kubwabwaja.

    Mdau TML

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2012

    HONGERA ZENU MAHARUSI, HAKIKA NAKUMBUKA JINSI REV. KADIVA NA BISHOP MALASUSA WALIVYOKUWA WANAKUTANIA UKIWA KAMA MZEE WA USHARIKA ULIYEKUWA HUJAOA. PIA WASHARIKA WA AZANIA TULIVYOSHANGILIA ULIPOSEMA UNAKWENDA KUSOMEA UCHUNGAJI. MUNGU AIBARIKI NDOA YENU NA KAZI YA UCHUNGAJI, DADA HUYU AWE MAMA MCHUNGAJI MWEMA ATAKAYEFANYA KAZI YA MUNGU ULIYOITIWA ISONGE MBELE. HAKIKA NIMEFURAHI LEO KUONA NDOA HII.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2012

    Kuna Watu WAMEBARIKIWA FULU, Kwa kuongeza hapo juu mdau, Hata mdhamini wake alikuwa ni Mchungaji Thomito; alishatwaliwa Mungu amlaze Pema peponi. Ki ukweli wala sishangai Haruc yake kufungwa na Askofu; Ningeshanga isingefungwa na Askofu. Hongereni sana Maharusi. Mungu awalinde Amen.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2012

    Kuna watu wakali humu? Sasa wewe mchungaji mtarajiwa nani alikwambia ule hilo tunda kabla ya ndoa? Naona yule anayejibu atajibu fasta kama vile alikuwepolikiliwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...