Pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouuds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akiwa na sehemu ya uongozi wa juu wa kampuni hiyo,wakifanya mazungumzo mafupi na Uongozi wa chama cha CHADEMA,ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw.Freeman Mbowe ambaye aliongozana na Mbunge wa jimbo la Ubungo,Mh John Mnyika pamoja na Ofisa Habari wa chama hicho,Bw.Tumaini Makene,na kufanya ziara fupi ya kuitembelea kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo,mapema leo asubuhi,Mikocheni jijini Dar.
Mh.Freeman Mbowe akiwa ofisini kwa Bw.Joseph Kusaga wakizungumza machache mara baada ya kuwasili mapema leo mchana ndani ya mjengo wa kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.
Mwenyekiti wa CHADEME,Mh.Freeman Mbowe akizungumza na Mbunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho,Mh John Mnyika ambaye aliambatana na Ofisa habari wa chama hicho,Bw.Tumaini Makene,ndani ya ofisi ya Bw, Joseph Kusaga,Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake,Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mh Freeman Mbowe mapema leo mchana kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.Picha zaidi Bofya hapa






Ndugu Kusaga vipi umeshatimiza timu ya watoto? Naona unaiweka simu pahala pabaya, tumia meza ndugu yangu baadae isiwe ishu!
ReplyDeleteSafii, ebwana sasa nawakubali chadema...haiwezekani yule mwehu msichana anatumia vyombo vya habari kuchafua majina ya watu!! viva chadema na km vp mshitakini tu
ReplyDeleteHivi nilidhani lile gari la kiongozi rasmi wa upinzani ulilisusa ? kumbe bado unalo! safi sana
ReplyDeleteNimependa sana majibu ya Mbowe. Ameonyesha ukomavu wa hali ya juu.
ReplyDeleteHaitakuwa rahisi kuivuruga CHADEMA kama wanavyofikiri, CHADEMA wamejipanga fresh.
Kaka michuzi hebu urudishe nyuma huo mkokoteni wa mjasiriamali wenye alama za VX, LAN, na kibao cha njano chenye K.
ReplyDeletehalafu mbona yule mbwabwajaji kwenye jahazi jana alikimbia na kusingizia anaumwa.? au aliona soo anavyowa kandya CDM?
ReplyDeleteKUB:
ReplyDeleteAhhh wapi, Mhe. Mbowe kuirudisha Serikalini VX V8 mchezo?
Kwanza alikuwa anasali sala zote afikie hapo alipo na ndio amefikia ukomo wa mwisho kabisa na kwake ndio kama ameshaupata Uraisi wenyewe aliokuwa anauota na kumkosesha usingizi hapo kabla!, (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI), sasa amefika afanye nini tena?
alikuwa anatishia Mnyau tu yule!